Ni kawaida kwa mzazi akiwa na mtoto zaidi ya mmoja,
kuwalinganisha hasa tabia zao, tangu pale walipozaliwa., Utakuta huyu alikuwa
analia sana , labda huyu alikuwa analala sana huyu ni mpole au huyu ni mtundu
n.k
Hata hivyo watoto hao wanapozidi kukuwa tabia na
maumbile yao huzidi kutofautiana siku hadi siku. Mara nyingi muonekano wao hutofautiana kiasi kwamba ni vigumu kutambua kuwa ni watoto wa mama na
baba mmoja.
Katika miaka mingi watafiti wemegundua kuwa kuna uhusiano
mkubwa wa tabia za watoto na mpangilio wa kuzaliwa. Kwa mfano watoto wa kwanza
kuzaliwa,mtoto wa pili, na wamwisho.
Mtoto wa kwanza.
Mtoto wa kwanza katika familia mara nyingi anawajibika juu
ya wenzake,anakuwa na mpangilio wa mambo yake,huwa anafanikiwa katika mambo
yake, na huwa anonyesha mfano mzuri wa kuwa kiongozi mbele ya wadogo zake. Yeye
huwa anakuwa ndiye kinara wa tabia njema au anayefanya vitu ambavyo wazazi huwa
wanapenda, na mara nyingi anafanya hivyo kama mfano kwa wadogo zake.kama kuna
watoto wadogo hapo nyumbani mtoto wa kwanza anakuwa kama yeye ndio mlezi na
wadogo zake wanapenda kujifunza kutoka kwake
Mara nyingi wanakuwa na malengo ya kufanya vizuri shuleni na
marazote wanapata mafanikio kwa sababu wanajitahidi sana.Kwa bahati mbaya mara
nyingine kwa sababu ya kutaka sana kufanikiwa kunamsababishia msongo wa mawazo
ambao si vizuri sana kwa watoto.
Mtoto wa kati
Mtoto wa katikati mara nyingi anachukuliwa kuwa mtoto mgumu
sana kumuelewa, Mara nyingi mtoto huyu hapati nafasi ya kupendwa kama
alivyokuwa mtoto wa kwanza au wa mwisho, huwa anaona anatengwa na ni vigumu sana
kwake kuona ni mwelekeo upi aende. Na mara nyingi anakuwa na mtazamo tofauti wa
nini afanye au nani awe, ili kujitofautisha na mkubwa wake, na mara nyingi huwa ni mtafiti na huwa
anapenda kujaribu vitu ambavyo ni vigumu kujua matokeo yake.
Mtoto wa mwisho
Mtoto wa mwisho ni mtoto wa familia, ni mtoto ambaye kila
mmoja ndani ya familia anawajibika kumuangalia. Wazazi wanapenda kumpendelea na
mara nyingi zile sheria wazazi walizoweka huwa kwa mtoto huyu wa mwisho
azizingatiwi tena.
No comments:
Post a Comment