MPAKA UNIPE ELA!!!
Wazazi sijui tunakwenda wapi, inamaana tunaruhusu mtoto kuwa ombaomba bila sisi mwenyewe kufahamu, Ilo neno” mpaka unipe” ela ni mara nyingi sana kuwasikia watoto wakidai kutoka kwa wazazi wao.
Unaweza kuta mzazi anamtuma mtoto, labda anamwambia kaoshe vyombo basi, mtoto atakataa na baadae atasema ukunipa pesa nitaosha, au ukininunulia icecream nitaosha, na mzazi utakuta anakubaliana na ombi hilo
.
Sawa sikatai tunawapenda watoto wetu sana ila, tuangalie ni mahali gani na wakati gani pa kutoa pesa kama reward au zawadi.
Ukichukulia watoto wa miaka 7 na kuendelea awe wa kike au wa kiume ni umri ambao tunapaswa kama wazazi kuwafundisha shughuli ndogondogo pale nyumbani, na haitakuwa busara hata kidogo kumpatia pesa mtoto akisha fanya au kabla hajafanya kazi yoyote utakayomwambia aifanye. Unachotakiwa kama mzazi ni kumueleza umuhimu wa kujifunza kazi hizo, moja ni kuonyesha kuwa anawajibu wa kusafisha mazingira aliyopo, kusafisha chumba chake, kuondoa vyombo mezazani, kuandaa meza, kutandika kitanda chake mara aamkapo, na mambo mengine madogo madogo.
Na pia wewe mzazi ujivunie kuwa anaweza kufanya hivyo bila kupewa pesa, ilishawahi tokea binti ameolewa mahali fulani, na kwa bahati nzuri au mbaya binti yule wazazi wake walimpenda sana kiasi kwamba hakuwa anafanya shughuli yoyote alipokuwa nyumbani pa wazazi wake.
Sasa binti yupo kwa mume hajui kupika , na mumewe anataka chakula alichopika mkewe, unajua ilimsumbua sana Yule binti, na hata siku mmoja alitamka “Namlaumu sana mama yangu kwa kunilea vile, hebu ona mimi ni mwanamke aina gani nisiyejua kupika, hakuwahi kunifundisha kupika ati alinipenda sana kila kitu alikuwa anafanya yeye mwenyewe ona sasa naaibika.
Hayo ni maneno ya kusikitika kwa huyo binti, naomba wazazi tuchukulie huo mfano kama changamoto kwetu, hebu tuwafundishe watoto wetu kazi ndogondogo majumbani mwetu.
No comments:
Post a Comment