MFUNDISHE MTOTO KURUDISHA KITU AMBACHO SI CHAKE
Wazazi watoto wetu wanapokuwa mashuleni huwa wanachukuliana
vitu vyao, mfano mtoto wangu siku moja alikuja na saa ya rafiki yake,
nikamuuliza mbona una saa ambayo si yako, akasema nilimuomba rafiki yangu
akanipa nivae, tena amesema ni yangu kabisa. Ukweli ni kwamba ilibidi nimwambie
mtoto wangu amrudishie rafiki yake saa yake kwani saa ile si yake. Na pia
nikamwambia wazazi wake watamuuliza saa yake iko wapi
Kwa mfano huo naomba wazazi tushirikiane na walimu, kwani mara mtoto
akipoteza kitu chochote, nafikiri kitu cha kwanza cha kufanya utamuuliza mwalimu
wa darasa na ikitokea shuleni hutapata majibu ya kuridhisha utakuwa huna la
kufanya. Kumbe ungemdadisi mtoto kwamba umempa nani saa, au kitu chochote
kilichopotea angekwambia amepotezea wapi
Wazazi mtakubaliana na mimi mara nyingi watoto wetu wanapoteza
vitu kama penseli, ruler, kichongeo na chupa za juice, folder na n.k .
Utajikuta unanunua vitu hivyo mara kwa mara mpaka unachoka na katika hali ya
kawaida hutaweza kumwacha mtoto aende shule bila kalamu au ruler hivyo utakuwa
unanunua mara kwa mara. Hii ni changamoto
kwa mzazi na mwanae wa shule, ikiwa ni pamoja na kumuuliza mtoto na
kumfundisha jinsi ya kutunza vitu vyake, na kumfundisha kukumbuka kuchukuwa
kalamu au saa yake ikiwa amempa mwenzie au rafiki yake. Kingine cha msingi ni
sisi wazazi kuwachunguza watoto wetu ikiwa wamekuja na vitu ambavyo si vyao na
kumshauri kurudisha kwa rafiki au mwenzie aliye vichukuwa kwake.
Ili kwa kiasi kupunguza upotevu wa vitu vya
shule kwa watoto wetu ni kufuatilia na kuwafundisha jinsi ya kutunza vitu
vinavyowahusu, pia kumchunguza mwanao anapokuja na kitu ambacho si chake kumshauri
akirudishe shuleni na kumpatia mwalimu. Kwani walimu huwa wanakuwa na taarifa
za upoteaji wa vitu vya wanafunzi hivyo inakuwa rahisi pia kwao tukishirikiana
nao kwa namna hiyo
No comments:
Post a Comment