Subscribe:

Ads 468x60px

Monday, April 2, 2012

Is it only my husband?


Jamani na nyie waume zenu wapo kama wangu? It’s now three months tangu nimejifungua mtoto wangu wa kwanza, nimeolewa na ninampenda mume wangu. Ila jamani du… yani kama vile mtoto huyu ni wa kwangu mwenyewe. Akitoka kazini analala chumba chake wakati mie nahangaika na mtoto usiku kucha na anasikia anavyolia bila kuona msaada wake… nimejaribu kumwambia anasema yeye anawahi kazini asubuhi mimi siendi kazini bado. Hivi hii ni kawaida ? Kwa sababu nachoka eti jamani… inakera lo!
send your challenge for discussion at (momntoto@yahoo.com) we shall post it for discusion

Wadau michango ni mizuri so far; tuendelee kusaidiana, some wanasema wanaume wanaogopa watoto wadogo ndio maana wanakua hawatusaidii early days after delivery, wengine wanasema hawana experience, na wengi wanasema tuwe wawazi kuwaambia watusaidie;
   Bado swali lipo kwamba ni kweli hizi sababu ndo toshelezi za kuwafanya wanaume wasiwe wa maana sana wakati sie bado tunaumwa na tunaitaji misaada yao? Eti ni kweli ni kwa sababu ya uoga wa watoto wachanga kweli kweli?... is it ukosefu wa huruma katika mioyo yao au ni nini? na ni kwa nini wengine wanaweza wengine hawawezi? au ndo tunakua hatujapendwa vizuri sie?

Tufanye nini kurekebisha segment hii kubwa ya wanaume hawa?......

5 comments:

Anonymous said...

Best mimi naoana wako anaafadhali, mimi niliambiwa nikae kwanza kwa mama yangu mzazi, mpaka miezi mitatu iishe, kwani yeye hana uzoefu, eti mtoto akiugua usiku tutafanyaje?

Basi ilibidi nikae huko kwa miezi hioi mitatu ndio nikarudi kwangu, kwa kweli nilisikitika sana kwani niliona kama namtwisha mama yangu mzigo, sasa nini maana ya kuwa mume namke, nilitegemea mimi na yeye ndio tungeshirikiana kujifunza wote pamoja kumlea mtoto wetu wa kwanza lakini haikuwa hivyo.

Anonymous said...

Mwenzangu, kwa wamasai ndo balaa! baba anatakiwa kuwa mbali na mke akishajifungua kwa muda wa miaka miwili.

Anonymous said...

Bora hata wewe, mwingine hata huyo mtoto akilia utasikia unaambiwa yaani wewe ujui kama mimi nawahi kazini kesho asubui!! embu mnyamazishe huyo mtoto wako , hilo neno "huyo mtoto wako" ndo linakera zaidi

Anonymous said...

jamani poleni sana, mimi ninabahati mume wangu ananisaidia sana katika kipindi hicho tunabembeleza wote usiku kutwa hata anakwenda kazini anasinzia. Anatakiwa akusaidie kama hawezi basi awepo mtu mwingine wa kusaidia

Anonymous said...

Mimi naona ni baadhi ya wanaume, lakini ni uoga tu mimi nafikiri wakizoea watakuwa wanasaidia, kuna msemaji mmoja hapo juu amesema mume wake anaogopa mtoto akiumwa nani atawasaidia.Unajua wanaume wengi ni waoga katika kulea hivyo ukimshirikisha uoga utaisha.

kitu cha msingi unatakiwa umueleze kwamba, wewe huendi popote na ni lazima akusaidie kwani wote wewe na yeye wote ni wazazi wapya au sio jamani,
Usimuogope mume wako inabidi umuheshim na yeye akuheshimu. hivyo sema usikike.

Post a Comment