KUNA UHUSIANO GANI KATI YA URIJALI NA KITOVU CHA MTOTO,
Nimesikia wazazi mbalimbali wakiongele swala la kitovu cha
mtoto mchanga kudondokea kwenye uume wa mtoto kuwa unaleta madhara hapo baadae,
Eti wanasema mtoto huyo ambaye kitovu chake kilidondokea kwenye uume wake
atakuwa si rijali je kuna ukweli hapo?
Pia nimeona wazazi walimuwekea kidoti cheusi mtoto mchanga
kwenye paji ati, kuzuia kwikwi inahusu vipi? Kumvalisha mtoto kitambaa chausi
mkononi au kiunoni jamani inakuwaje, zaidi ya yote mtoto akiwa na kikoozi
ambacho hakijapona kwa muda kidogo wanasema anakimeo?
Inakuwaje wewe mama umetoka kujifungua na unapelekwa kwa
wazazi wako ati ukale uzazi kwa muda wa miezi 3, na huyo baba uliye zaa naye
unamwacha ati hana uzoefu, kwani wewe unao, huoni kama unawasumbua wazazi wako,
wakulee wewe na kisha wakulelee mwanao na zaidi ya yote ukae huko miezi zaidi
ya 3 , sasa huyo baba mtoto atajua lini kulea mtoto mchanga, Baadhi ya watoto
wachanga huwa wanalia sana usiku hivyo vilio huyo baba takuwa amevisikia saa
ngapi kwake inakuwa ni adithi tu, mtoto ni wenu wote lakini kusota usiku
kubembeleza mtoto usote mwenyewe na wazazi wako hebu fikiria. Kuna baadhi ya
akina baba hawataki hata kuwashika watoto wao ati wanadai wanaona kama
wanawaumiza jamani hutaki kushika mtoto wako mwenyewe?
Mimi ninaonelea hivi, mara mtu unapojifungua maadamu
umeolewa na mumewako yupo hapo ni vizuri ukae hapohapo na usiende popote,
mujifunze wote kwa pamoja kumlea mtoto wenu. Wewe mama unatakiwa ufanye juhudi
za makusudi kumshirikisha mumeo sio unaambiwa tu nenda kwa mama ndio anajua na
wewe unakubali, Ikiwa mtahitaji msaada wa kulea ni bora msaidizi huyo aje hapo
kwako na akuelekeze nakisha aende. Zaidi ya yote madakitari wa watoto wapo kila
kona hivyo usihofu kuwa jasiri.
No comments:
Post a Comment