MWANAO ANAJUA KUAMKIA NA KUSEMA ASANTE,
Katika mila na
desturi zetu watanzania tunatakiwa kuwafundisha watoto wetu tabia ambazo
zinakubaliwa na jamii zinazotuzunguka. Moja ya tabia hizo ni tabia ya kusalimia,
na kusema asante.
Kwa kweli usipomfundisha mtoto wako angali mdogo tabia hizi
itakuwa ni vigume kuzifanya anapokuwa na umri mkubwa au hata kama atakuwa
anasalimia ni mpaka akumbushwe. Hivi umeshawahi kutana na rafiki au jamaa na
mtoto anakakataa kusalimia , unajisikiaje kweli inatia aibu mwenzenu yalinikuta
.
Kwa kweli inapendeza sana mtoto anapokuwa na tabia nzuri,
inapendeza pale unapompatia zawadi, au unapomfanyia kitu mtoto akasema asante,
au nyie mwaonaje , Mimi imenisumbua sana kwa mtoto wangu alikuwa hawezi
kumsalimia mtu bila kumwambia , mara nikutanapo na rafiki ,jamaa au ndugu kweli
ilikuwa inani aibisha kwani ni mpaka aambiwe hujambo, ndio naye atajibu sijambo, halafu inabidi
umwambie tena sema shikamoo, ndi atasema shikamoo, kweli inatia aibu.
Sasa basi siku mmoja akaniuliza hivi mama how do you say
shikamoo in English?
Kwa wenzetu wa ulaya wanapenda sana kusema sorry au, neon
please, au kindly, au excuse me, haya ni maneno mazuri ya kuonyesha unyenyekevu
na kujali mtu mwingine, mara nyingi mtumiaji wa maneno haya, anatumia pale
ambapo anataka kufanya jambo au afanyiwe jambo, lakini anajua wazi kitu
atakachokifanya kinaweza kisiwe kizuri kwa mtu mwingine, au kikamkwaza mtu
mwingine, hivyo kwa kujali hali hiyo na
ndio maana atatumia maneno haya.
Kwetu sisi pia kuna baadhi ya watu wanayatumia maneno haya pia pale tu
anapozungumza kiingereza ila anapozungumza Kiswahili mara nyingine watu
wanajisahau kutumia maneno kama haya ambayo ni, samahani, tafadhali,
No comments:
Post a Comment