MAMA AKIWA NA KIPATO KIKUBWA KULIKO BABA KATIKA FAMILIA NI TATIZO,
Katika pitapita zangu, nime gundua kuwa mama akiwa na kipato
kikubwa kuliko baba katika familia ni tatizo kubwa kwa kwa baadhi ya familia.
Binafsi nime shuhudua mama akijishusha sana ili kuchukua
nafasi yake ya kuwa mtiifu kwa mume wake hata kama kipato chake ni kikubwa
kuliko cha mume wake. Lakini basi bado inakuwa ni tatizo kwani mume Yule mwenye
kipato kidogo bado anajisikia kutawaliwa, kutoheshimiwa na kudharauliwa.
Mwingine anakuwa mkali na kudiriki kusema au kwa vile wewe unapata pesa nyingi,
naona hunieshimu hata kidogo, Wanaume hawa wanakuwa walalamishi sana hata
ukifanya kitu kidogo cha maendeleo
nyumbani basi atalalamika hujanishirikisha,
Kuna baadhi ya wanaume huchukua nafasi hii ya kutoelewana na kuanzisha
mahusiano mengine ya familia na mwanamke mwingine ambaye yeye anajiona kuwa juu
zaidi kipesa, sasa basi anaishia kuwa na familia mbili yaani ya kwa mke wake wa
ndoa ambaye kwake yeye anamfanya benki anakuwa anachukuwa pesa na kwenda
kuilea ile familia ndogo aliyonayo. Hebu tuchangie hili .
No comments:
Post a Comment