Subscribe:

Ads 468x60px

Tuesday, April 17, 2012

JE MWANAUME NI MTOTO ASIYEKUWA?


JE WAJUA BABA ZETU, WAUME  ZETU NI WATOTO WASIOKUWA????

Hivi wenzangu mmejaribu kufikiria kwa nini wanaume zetu ni kama watoto  wasio kua?


Mpaka  hivi leo wewe kama mama ukirudi nyumbani utatakiwa kumuhudumia mumeo kama vile unavyomuhudumia mtoto wako.

Tulipokuwa wadogo, wazazi wetu walituhudumia kwa kila kitu, ikiwa ni pamoja na kutupa malezi bora , kutupeleka shule, na  kutupatia vitu vingine vingi ambavyo kama wazazi walitufanyia sisi watoto  kwa  upendo. Japokuwa kuna baadhi ya wazazi   ambao kwa bahati mbaya hawakuwa wanachukuwa nafasi zao za kuwalea watoto wao waliowaleta hapa duniani kwa pamoja yaani, wazazi wote wawili.   wapo baadhi ya wazazi waliowatelekeza watoto na  mama zao au wengine walio watelekeza watoto na baba zao.

Sasa basi kwa wale walitelekezwa na mzazi mmojawapo yaani baba au mama huwa wanapata taabu sana katika makuzi yao, wanashindwa kujua umuhimu wa Yule mzazi aliyemtelekeza.  Wengi wa waathirika wa tatizo hili huwa wanafikiria kulipiza kisasi kwa mzazi aliyemtelekeza, kwa kutomtunza kama mzazi na kumpatia mahitaji yake muhimu pindi anapokuwa na fedha zake na uwezo wa kumsaidia mzazi wake huyo, aidha mama au Baba .

Kwa asilimia kubwa akina baba ndio wanaoongoza katika  kutelekeza  familia zao yaani mama na watoto . Hivyo basi kama kawaida ya mama ambaye kwa sehemu kubwa ndiye  mlezi wa familia ndiye  atahangaika sana kwa kuwalea watoto wake, na mara nyingi watoto watakuwa karibu sana na mama yao kwa kumfariji na kumuhaidi kuwa watafanya vizuri shuleni ili watapokuwa wakubwa wakipata kazi watamtunza kulipia yale yote aliyoyafanya kwaokama fadhila.

Na kweli mungu huwa anawabariki watoto hao kwa nafasi zao mbali mbali, na hapo ndipo utaona baba anajitokeza na kuanza kuwatambua watoto na kuanza kuomba msaada lakini sasa inakuwa vigumu sana kwa mzazi huyo kupata msaada, kwani yeye ndiye aliyewatelekeza hapo awali na huwa hawaoni sababu ya kumsaidia. Hapo sasa mama anabidi atumie busara zake tena kuwaambia watoto wake umuhimu wa kumsaidia tena baba yao na kumpatia nafasi baba yao katika maisha yao
.
Kama Ujuavyo mama anaweza vyote, Japokuwa ni mama huyo aliyelekezwa na watoto  akaangaika kwa taabu sana  kuwalea na kuwasomesha mpaka watoto wamefanikiwa, bado tena ni mama huyohuyo anayewasihi watoto kumsamehe baba yao ili waanze kumpenda na kumtunza kama wanavyomfanyia yeye. Hapo sasa ndio tunapata usemi ule kwamba mwanaume ni mtoto asiyekuwa kwani mama ameshalea watoto wameshakuwa lakini mpaka leo bado anamlea mume wake, kwa kuwa mtetezi wake kwa watoto aliowatelekeza, kwa kumfulianguo zake, kwa kumuandalia chakula chake,na zaidi ya yote kumpenda zaidi .

3 comments:

Anonymous said...

Ni kweli kabisa wanawake wana mioyo yenye huruma, kwani wanasema mtoto akiunyea mkono wako utaukata na kuutupa? la hasha, utasafisha tu, ndivyo hivyo hivyo tunavyowafanyia wanaume kwani ndio watoto wetu.

Anonymous said...

mimi naona wanaume ni kubwa jinga!!!!????????

Anonymous said...

Kwa karibu mwaka mmoja, mume wangu aliniacha mimi na watoto wetu wawili. Aliacha kujali, akaacha kupiga simu, na akaondoka kabisa. Nilikuwa nimevunjika moyo, nimechanganyikiwa, na karibu kupoteza tumaini. Kisha siku moja, rafiki yangu aliniambia kuhusu Dkt. Dawn, mtu wa kiroho aliyepewa kipawa na ulimwengu ili kuwasaidia watu kurejesha upendo na amani.

Mwanzoni, nilikuwa na shaka, lakini kitu kuhusu maneno yake kilinipa amani. Aliniambia haswa kilichokuwa kibaya na kwamba mtu alikuwa ametupa uchawi mkali kututenganisha. Aliandaa kazi maalum ya kiroho na uchawi wa kuungana tena kwa ajili yangu - na ndani ya siku chache, mume wangu alinipigia simu ghafla, akilia na kuomba msamaha.

Tangu wakati huo, maisha yangu hayajawahi kuwa sawa. Ndoa yetu sasa ni tamu na yenye furaha zaidi duniani. Tunapendana zaidi kuliko hapo awali, na nyumba yetu imejaa vicheko na baraka.

Lakini sio hivyo tu - Dkt. Dawn pia alisaidia kuondoa bahati mbaya na nishati hasi iliyozunguka familia yetu. Tangu wakati huo, kila kitu kimekuwa laini: amani nyumbani kwetu, maendeleo ya kifedha, afya njema, na furaha safi.

Ninashukuru ulimwengu kila siku kwa kuniongoza kwa Dkt. Dawn. Kwa kweli ni mtu mwenye nguvu na mwanga wa kimungu. Ikiwa unapitia hali yoyote - huzuni, bahati mbaya, au kuchanganyikiwa - usikate tamaa. Mfikie na uache ulimwengu ufanye kazi kupitia yeye ili kubadilisha hadithi yako, kama vile alivyobadilisha yangu.

Wasiliana naye kwenye WhatsApp: +2349046229159
dawnacuna314@gmail.com

Post a Comment