JE WAJUA BABA ZETU, WAUME
ZETU NI WATOTO WASIOKUWA????
Hivi wenzangu mmejaribu
kufikiria kwa nini wanaume zetu ni kama watoto wasio kua?
Mpaka hivi leo wewe kama mama ukirudi nyumbani utatakiwa kumuhudumia mumeo kama vile unavyomuhudumia mtoto wako.
Mpaka hivi leo wewe kama mama ukirudi nyumbani utatakiwa kumuhudumia mumeo kama vile unavyomuhudumia mtoto wako.
Tulipokuwa wadogo, wazazi wetu walituhudumia kwa kila kitu, ikiwa ni pamoja na kutupa malezi bora , kutupeleka shule, na kutupatia vitu vingine
vingi ambavyo kama wazazi walitufanyia sisi watoto kwa upendo. Japokuwa kuna baadhi ya wazazi ambao kwa bahati mbaya hawakuwa wanachukuwa nafasi zao za kuwalea watoto wao
waliowaleta hapa duniani kwa pamoja yaani, wazazi wote wawili. wapo baadhi ya wazazi waliowatelekeza watoto na mama
zao au wengine walio watelekeza watoto na baba zao.
Sasa basi kwa wale
walitelekezwa na mzazi mmojawapo yaani baba au mama huwa wanapata taabu sana
katika makuzi yao, wanashindwa kujua umuhimu wa Yule mzazi aliyemtelekeza. Wengi
wa waathirika wa tatizo hili huwa wanafikiria kulipiza kisasi kwa mzazi aliyemtelekeza, kwa kutomtunza kama mzazi na kumpatia mahitaji yake muhimu pindi anapokuwa na fedha zake na uwezo wa kumsaidia mzazi wake huyo, aidha mama au Baba .
Kwa asilimia kubwa
akina baba ndio wanaoongoza katika kutelekeza familia zao yaani mama na watoto . Hivyo basi kama kawaida ya
mama ambaye kwa sehemu kubwa ndiye mlezi wa familia ndiye atahangaika sana kwa kuwalea watoto wake, na mara nyingi watoto watakuwa karibu
sana na mama yao kwa kumfariji na kumuhaidi kuwa watafanya vizuri shuleni ili
watapokuwa wakubwa wakipata kazi watamtunza kulipia yale yote aliyoyafanya kwaokama fadhila.
Na kweli mungu huwa
anawabariki watoto hao kwa nafasi zao mbali mbali, na hapo ndipo utaona baba
anajitokeza na kuanza kuwatambua watoto na kuanza kuomba msaada lakini sasa
inakuwa vigumu sana kwa mzazi huyo kupata msaada, kwani yeye ndiye
aliyewatelekeza hapo awali na huwa hawaoni sababu ya kumsaidia. Hapo sasa mama
anabidi atumie busara zake tena kuwaambia watoto wake umuhimu wa kumsaidia tena
baba yao na kumpatia nafasi baba yao katika maisha yao
.
Kama Ujuavyo mama
anaweza vyote, Japokuwa ni mama huyo aliyelekezwa na watoto akaangaika kwa taabu sana kuwalea na kuwasomesha mpaka watoto
wamefanikiwa, bado tena ni mama huyohuyo anayewasihi watoto kumsamehe baba yao
ili waanze kumpenda na kumtunza kama wanavyomfanyia yeye. Hapo sasa ndio
tunapata usemi ule kwamba mwanaume ni mtoto asiyekuwa kwani mama ameshalea
watoto wameshakuwa lakini mpaka leo bado anamlea mume wake, kwa kuwa mtetezi
wake kwa watoto aliowatelekeza, kwa kumfulianguo zake, kwa kumuandalia chakula
chake,na zaidi ya yote kumpenda zaidi .
2 comments:
Ni kweli kabisa wanawake wana mioyo yenye huruma, kwani wanasema mtoto akiunyea mkono wako utaukata na kuutupa? la hasha, utasafisha tu, ndivyo hivyo hivyo tunavyowafanyia wanaume kwani ndio watoto wetu.
mimi naona wanaume ni kubwa jinga!!!!????????
Post a Comment