Mila na desturi zetu tuliowengi,hapa Tanzania zinafanana, hasa pale binti anapoolewa au anapooa huwa anapewa ushauri, na wazazi, ndugu na marafiki waliomtangulia kwenye upande huo wa kuoa na kuolewa.
Lakini basi mama na mwana huwa wanakuwa na faragha zaidi kuongelea swala hilo kwa undani, kwani kama ni binti nafikiri utafunguka zaidi kumueleza mama yako wasiwasi au hofu yoyote uliyonayo, na mara nyingi mama yako atakupa ushauri au jinsi ambayo ukiitumia katika maisha yako ya ndoa, ndoa yako itadumu sana.
Napenda kushirikiana na wewe katika mjadala huu ushauri wangu alionipa mama yangu ambao kwao umeniwezesha kuishi na mume wangu na sasa ni zaidi ya miaka kumi,
( mama alisema unaolewa utakuwa na watoto mungu akipenda, utawapenda sana watoto wako, lakini usiache kumpenda mume wako, zaidi ya yote uipende ndoa yako, kwani bila kuwa na maelewano na mwanandoa mwenzio, ndoa yako haitadumu.) Mwanamke mpumbavu huivunja ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe.
Je wewe mama yako alikuambia nini? hebu tushirikishe
No comments:
Post a Comment