MTOTO WA NJE YA NDOA NI NANI,
Mtoto aliyezaliwa baada ya wazazi au mzazi wake kufunga ndoa
ni mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa, hii haimualalishi mtoto huyo kuwa mtoto wa ndani ya ndoa hata
kama wazazi wake waliomzaa watakuja funga ndoa baadae.
Kumbe ndio maana utaona watu wengi waliochumbiana, wanafunga
ndoa hata kama wamekwisha peana ujauzito, Wapo wale wanosubiri mwenzi wake
ajifunguo ndio afunge ndoa, ni jambo zuri lakini sijui kama unafahamu kuwa,
utakapo mzaa huyo mtoto na kisha uende ukafunge ndoa, mtoto utakaye mzaa ni mtoto
wan je ya ndoa hata kama uliyefunga nae ndoa ndiye baba wa mtoto huyo.
Unaweza kuwa mmoja wa waliojifungua kwanza
, na kisha kufunga ndoa swali langu ni kwamba kisheria kuna njia yoyote ile ya
kumualalisha mtoto huyo uliyemzaa kabla hujafunga ndoa ili naye awe mtoto wa
ndoa?
Inapendeza na ni vizuri kuwa na watoto wote ndani ya ndoa
,ila kunakuwa na sababu nje ya uwezo wa mtu zinazopelekea kuzaa nje ya ndoa,
lakini pia huenda kuna njia ya kurekebisha hali hiyo, yaani kumhalalisha mtoto
huyo wan je ya ndoa ,kama kuna mtu yeyote anayefahamu ni namna gani tunaweza
kumhalalisha mtoto wan je ya ndoa tunaomba ushauri wako.
UMEKISAJILI CHETI CHAKO CHA NDOA?
Wengi wetu tunafahamu kuwa ukishafunga ndoa halali, kwa
wakristo au waislam ni lazima utapatiwa cheti cha ndoa. Ni uthibitisho kwamba
watu wawili hao ni mke na mume. Lakini kumbe
vyeti hivyo vinatakiwa pia kusajiliwa na serikali, hivyo basi mume au
mke unatakiwa uvipeleke vyeti hivyo kwenye ofisi za Wakala wa Usajili na
Udhamini (RITA) huko sasa vinasajiliwa tena.
Kwa kufanya hivyo unakuwa na uhakika ya kuwa ndoa yako
inatambulika pia katika serikali ya nchi yako, na pia inasaidia sana kwa
kutunza kumbukumbu ambazo kwa sababu mbalimbali za kudai haki hasa kwa akina
mama, endapo kuna tatizo la kisheria utakalokuwa nalo.
Mimi ni mwenzenu nilikuwa sijui, lakini baada ya
kufahamishwa nilikwenda kusajili cha kwangu inabidi niwashirikishe na nyie pia,
wewe mama ambaye ndiye unayetunza Documents zote hapo nyumbani kwako chukuwa
hatua na ue nde RITA.
No comments:
Post a Comment