MWANANGU ANAKOJOA KITANDANI , ANA MIAKA 12, NIFANYEJE,
Kitendo cha mtoto kukokoa kitandani akiwa na umri wa miaka
zaidi ya kumi kweli si kitu cha kupuuza ni vizuri kutafuta njia za kumsaidia
kuna njia amabzo mimi binafsi nimezitumia na zimenisaidia, na
nilipowashirikisha baadhi ya marafiki zangu zimewasaidia,
Moja wapo ya njia hizo ni ushirikiano hapo nyumbani, kati ya
mzazi na mtoto, unatakiwa kumshauri mtoto kutokula vitu vya majimaji masaa2
kabla hajaenda kulala, ikiwezekana anywe maji na vitu vingine kama soda au
juice masaa 2 kabla hajakwenda kulala,
Pia anatakiwa kabla hajalala kuhakikisha hana mkojo ndani ya
kibofu chake , namaanisha kwamba mtoto aende akakojoe kabla hajalala.
Pia ni vizuri usiku kuwe na mtu anakwenda kumwamsha ili
aende akakojoe,lada ni dada au mtu yeyeto ukishtuka usiku labda unakwenda kujisaidia
ni vizuri utumie wakati huo kumshtua naye aende kujisaidia.
Siku ikitokea kwa bahati mbaya amekojoa kitandani ni vizuri,
kumuelewa, na kwa hakika atajisikia vizuri ikimuelewa, kwani hata yeye mtoto
sidhani kama anapenda hali hiyo ya kujikojolea.
Kuna baadhi ya wazazi wanawapitisha watoto mitaani na
kuwatangazia kuwa wanakojoa kitandani, au pia wanawatangazia kwa marafiki zao
mashuleni au mtaani kweli hapo unakuwa ujamsaidia mtoto ila unamuaibisha tu.
Ukiangalia kwa undani hata mtoto mwenyewe hapendi kabisa,
ila inakuwa ni hali tu imejitokeza hivyo ni vema kumsaidia na si vizuri
kumuabisha kwani hali hiyo inamuumiza zaidi
1 comment:
Huyo sio kikojozi, mimi nina mtoto wa my sister ni kikojozi yaani nadhani ni doctor case, maana ana 5 yrs lkn akilala unaweza amshwa 6-7 times ndio hatakojoa, sasa inakuwa adhabu hata kwa yule aliye on duty wa kumwamsha, mtokeo yake anaachwa ajikojolee, mnaona ni bora kufua mashuka kuliko hiyo adhabu ya kumwamsha maana inakuwa almost wewe na mtoto mnakesha chooni..... nadhani hii ndio a kind of watoto vikojozi walivyo.. huo ushauri wako ni mzuri lakini ni 4 those wanaokojoa kibahati mbaya.
Post a Comment