Subscribe:

Ads 468x60px

Wednesday, April 4, 2012

UMRI WA KUMWANZISHIA MTOTO CHAKULA KIGUMU

Mtoto wako atakuwa tayari kuanza vyakula vigumu akiwa na umri wa miezi sita. usije akamwanzishia chakula kigumu akiwa na chini ya miezi sita, kwa sababu utumbo wa mtoto unakuwa haujaweza kusaga vyakula vigumu akiwa na miezi chini ya sita. Na pia anaweza kupata allegies.

Kwa kuanza unaweza kumtengenezea kiugali kilaini sana, tumia unga wa mahindi au mchele.

Ukiona ameshazoea unaweza sasa kumwanzishia kitu kingine, mfano mboga mboga na matunda,, Mfano mboga za majani mchicha na matembele,matunda kama papai, viazi vitamu, viazi mbatata na vingine kama maboga n.k.

Inashauriwa kutompa mtoto maziwa ya ng'ombe, asali na ute ule mweupe wa mayai mpaka afike mwaka mmoja.

kwa kuanza kumpa mtoto hicho chakula kigumu kinatakiwa kisagwe ama kwa kutumia blenda au kipekecho, hakikisha chakula hicho kinakuwa laini, Ila kila anavyozidi kukuwa unaongeza ugumu wa chakula hicho.

Unapomwanzishia mtoto chakula kipya ,unatakiwa umpe kwa siku 2 au3 mfululizo, ilikuguundua kuwa chakula hicho hakina madhara kwake hutaweza kugundua kama utampa kwa siku moja tu, madhara ninayo yazungumzia ni kama allegies.

kwa kuanza unatakiwa umpatie si chini ya vijiko viwili vya chai, uwe unaongeza kipimo kadri siku zinavyoongezeka. kama ikitokea mtoto hajakipenda chakula usikate tamaa, mwanzishie tena chakula hicho hicho alichokikataa siku nyingine tena mpaka atazoea.

Chakula cha mtoto hakitakiwi kuwekwa chumvi, sukari au viungo vyovyote, unatakiwa usafi wa kutosha wakati wa maandalizi ya chakula hicho

Kwa upande wa gharama , chakula kinachoandaliwa na mama nyumbani kina gharama kidogo kulinganisha na kile kinacho unzwa madukani, hivyo basi ili kupunguza ngarama ni vizuri kukiandaa chakula cha mtoto wewe mama mwenyewe.

Kumbuka( Babies don't need sweets not even a lollpop)

No comments:

Post a Comment