Subscribe:

Ads 468x60px

Sunday, May 6, 2012

KUNYONYA KIDOLE KWA WATOTO.


KUNYONYA KIDOLE KWA WATOTO

Kwa watoto wadogo, kunyonya kidole ni kitu kama cha kawaida vile, ingawa ni kwa watoto wadogo tu, wakati mwingine kunyonya kidole ni njia ya kumfanya mtoto apunguze njaa, ajibembeleze na kujisikia salama,mara nyingi mtoto ataacha  kunyonya kidole akiwa na umri wa miaka 3-6.

Hebu tujiulize kwa nini mtoto anyonye kidole?

Kwa watoto wengi wananyonya kidole kama mbadala wa kula chakula, au kupembelezwa na wakati mwingine ni kujiweka au kujisikia salama, ni kama tabia tu, ambayo mtoto alikuwa nayo tangu akiwa tumboni kwa mama yake, mara nyingi kunyonya kidole kunaletwa na hisia.
Kunyonya kidole kuna madhara kwa baadhi ya watoto watakaoshindwa kuacha kunyonya kidole kwenye umri wa miaka 4.
Inasababisha meno kutojipanga vizuri, wataalamu wa meno wamehusisha matatizo ya kuwa na meno yasiyo jipanga vizuri na kunyonya kidole. Kama mtoto atashindwa acha kunyonya kidole mpaka baada ya miaka 5, kuna uwezekanao mkubwa wa meno yake kutojipanga vizuri, kuota yamebebana, na kupata meno yanayo shindwa kungatana.

Jinsi ya kumsaidia mtoto ili aache kunyonya kidole.

Wazazi huwa wanapata wasiwasi mapema pale mtoto anaposhindwa kuacha kunyonya kidole.Inashauriwa kuwa usimfanye mtoto aache kunyonya kidole akiwa na umri chini ya miaka 4 isipokuwa tu pale utakapoona kuna tatizo linalojitokeza kwa sababu ya kunyonya kwake kidole.
Mara nyingi watoto wanaacha wenyewe kunyonya kidole, ikiwa hatatokea hivyo basi fanya kama hivi.
1.Pendelea kumpataia michezo amabayo itaufanya huo mkono anaonyonya wakati wote uwe busy, kama vile acheze puzzle, achezee toys ili mradi tu awe busy.
2.Akiwa amelala polepole kiondoe kidole mdomoni angalia usimwamshe.
3.Mpe mifano ya marafiki zake walioacha kunyonya kidole, ili umtie moyo nay eye aache.
4.Ongea naye juu ya bacteria wabaya ambao wapo kwenye mazingira ya nje amabayo kupitia kidole chake anaweza kuwapata.
5.Epuka kumwaibisha mbele ya wenzake, kwamba mchekeni jamani ananyonya kidole, usimwadhibu pia .
6.Usitumie njia ya kumtisha au kumwogopesha, kwani kunyonya kidole kwake inaweza kuwa ni emotional problem au anakuwa na stress  na anahitaji kufarajika. Hivyo ni bota kutafuta tatizo la stress na emotional problems zake na kuzitatua kabla hujamlazimisha kuacha kidole.

No comments:

Post a Comment