Subscribe:

Ads 468x60px

Monday, June 18, 2012

CHARITY BEGINS AT HOME


Charity begins at home,

Mwezi huu ulikuwa na sherehe nyingi  moja wapo ilikuwa ni siku ya mazingira duniani, hapa Tanzania pia tullisherehekea sana, ila mimi napenda kuisherehekea kwa kukumbushana jinsi gani tunaweza kuifanya miji yetu kuwa safi, ila napenda usafi wa miji yetu uanzie majumbani mwetu.

Nimekwisha sikia kuna baadhi ya mikoa hapa Tanzania inaongoza kwa kuwa na mazingira safi moja ya mikoa hiyo ni Kilimanjaro hasa mji wa moshi, na mwingine ni Mwanza, jamani Tanzania yetu hii ni kubwa sna ila miji miwili tu ndio imeonekana kuwa safi kweli hebu tubadilikeni.

Kwa kuanzia majumbani mwetu kwa kuwafundisha watoto wetu usafi, wakiwa nyumbani hata pia wakiwa wapo nje ya majumba yao, hii ikiwa ni pamoja na unapokuwa barabarani, au sheleni, Kumfundisha mtoto kutotupa takataka mpaka akutane na mahali penye dust bin, mimi ninahakika tukifanya hivyo tutakuwa na kizazi kisafi hapo baadae na pia nchi safi. 

No comments:

Post a Comment