Subscribe:

Ads 468x60px

Thursday, June 21, 2012

KIDALI PO!


UNAKUMBUKA  MICHEZO YA UTOTONI?

Wazazi wenzungu mnakumbuka michezo ile ya zamani kabla hakujawa na TV, Computer, Play Stations n.k Tulikuwa tunacheza michezo gani.

Mimi nakumbuka, mnakumbuka mchezo unaitwa kidali, kombolela, ready na kadhalika, kwa kweli ilikuwa ni michezo mizuri sana na tulikuwa tunaifurahia sana. Hivi umeshajaribu kuwafundisha watoto wako hii michezo, japo kwa kuwaeleza tu kuwa hapo zamani ulikuwa unacheza michezo aina gani?. Mimi nafikiri ni wakati umefika wa kuwafundisha watoto wetu michezo yetu ya zamani, kwani kwanza licha ya kuwa ilikuwa inafurahisha pia ni mizuri kiafya.

Nimewakumbusha hili kwa sababu hivi sasa kuna tatizo kubwa kwa watoto wetu, ambalo ni la kukaa ndani muda mwingi na kutazama TV, video game, play stations n.k. Tatizo hili lina madhara kiafya kwani watoto wengi wameanza kulalamika, macho kuuma, migongo kuuma ,shingo n.k.

Sasa basi sisi wazazi inabidi tufanye juhudi za makusudi kwa kuwatafutia michezo tofauti ya  kucheza, Michezo ya kujificha, kombolela, yai bovu na mengine mingi inabidi irudi jamani na wa kuirudisha ni sisi wazazi tulio icheza kwa kuwafundisha watoto wetu, Mnakumbuka kuruka kamba  sikuizi kuruka kamba ni mpaka uende Gim.
Maendele ni mazuri lakini tusipokuwa waangalifu watoto wetu tunao wapenda watakuwa wameathirika na maendeleo haya .

No comments:

Post a Comment