Subscribe:

Ads 468x60px

Thursday, June 21, 2012

KWELI NI MTOTO ASIYEKUWA


KWELI MWANAUME NI MTOTO ASIYEKUWA,

Nakumbuka tulishawahi kuongelea kuwa mwanaume ni mtoto asiyekuwa na kwamba wewe mke wake ni sawa na mama yake, rafiki yake na pia ni mke wake. Mwanaume akiwa nyumbani tegemeo lake ni kwa mkewe hasa kwa kila kitu, vitu kama chakula, nguo, usafi utunzaji wa document hasa zinazowahusu hapo nyumbani, vyeti vyake, hati ya nyumba, n.k.
Wanachojua maadamu mama yupo hapo nyumbani yeye ndiye muangalizi wa kila kitu, ataitwa kwenye interview  atakuja atakuuliza wapi vyeti vyangu, mnataka mkopo wa nyumba atakuuliza wapi hati ya nyumba, mnataka lipa bili wapi bili za maji n.k hivyo wewe mama unatakiwa kuwa smart kwani wewe ndiye unayetunza document.

Sasa imefikia hatua mungu amewajalia mnakiwanja mnataka kujenga, hapo tena ni sehemu nyingine wanaume wanahitaji msukumo kutoka kwa wake zao, kwani nimeona na ninaona jinsi ambavyo wanawake wanavyo wasukuma waume zao kuanza ujenzi na kufanya shughuli za maendele kwa ujumla.
Si maanishai wanaume wote wapo wale amboa wakiamua fanya jambo hufanya bila kusukumwa au kukumbushwa na wapo wale ambao wewe mama ukinyamaza tu kama ni mkopo mliuchukua utashaa utapoambiwa umekwisha na mjengo hauja anza. Kimsingi kila mtu amuangalie mwenzi wake na kujua ni mtu wa aina gani? Si vibaya wewe mama ukianza halafu yeye akafuatia, ikiwa unafanya kazi na mnachokiwanja na kila ukimwambia mwenzio tuanze kujenga naye anakuwa kama anapotezea wewe sasa chukua hatua, kama unapesa nunu nondo, mchanga, na kokoto ukiweza nunua na matofali, nakumbia kasha mchukue mwenzi na uende naye huko kwenye site yenu, Kesho yake yeye mwenyewe atatafuta fundi na ujenzi utaanza. 
Imeshatokea hivyo, lengo langu leo ni kukuhimiza wewe mama kuchukua hatua ya kuanzisha jambo ambalo mwenzio bado analivutia pumzi.

1 comment:

Anonymous said...

haswaaaaaaaaa!!!! wa mama tuwe front jamani sio lazima mpaka yeye aanze kujenga! na hawa wenzetu huwa wanapenda sana kusifiwa; jinsi walivyo na masifa akinunu kiwanja ukijidai kukiponda tu, ujue hicho kiwanja kinaweza kuuzwa bila hata wewe kujua, what they need is a word of encouragement.

Post a Comment