Ni Umri gani muhimu wa kumtairi mtoto wa kiume?
wazazi walio wengi huwa wanapata tabu kujua ni umri gani mzuri wa kumtairi mtoto, binafsi nilijaliwa kumtairi mtoto wangu akiwa na umri wa miezi miwili, japokuwa niliona nimewahi kumbe nilikuwa nimechelewa , Wapo walio watairi watoto wao wakiwa na siku 7 yaani kama Yesu.
Ukiwa bado hujamtairi mtoto wako mama bado hujachelewa, kunafaida za kumtairi mtoto wako mapema. Kwanza kabisa unamuondolea maumivu makali kwani akitairiwa akiwa mkubwa huwa wanaumia sana. Faida nyingine ni ya kiafya zaidi umewahi sikia watoto wadogo wakisumbuliw na infections kwenye mkojo mara nyingi, utapunguza sana ugonjwa huu ikiwa utamtairi mtoto wako mapema. Zipo faida nyingi hivyo tutaendele tena kukuletea topic hii.
1 comment:
Ashakum si matusi,mbona mimi nilisikia ukimtairi kabla ya kubaleghe utamuathiri mtoto kwa kumfanya uume wake uwe mdogo sana na kumsababishia matatizo ya kisaikologia maisha yote.
KK
Post a Comment