Familia pana au Kubwa,
Familia kubwa hii inamaanisha kuwa na familia zaidi ya mama ,baba na watoto.
Familia nyingi za kiafrika zinaishi na zaidi ya baba,mama na watoto wanasema kwa lugha ya kigeni extended families, Mimi ni mmoja ya watu tulioishi maisha ya namna hiyo nilipokuwa mdogo na mpaka nimeolewa bado naishi hivyo. kwa kifupi maisha ya namna hiyo ni kwa sabababu za umaskini au kipato kidogo kwa baadhi ya familia zetu .
wengi wetu tuliopitia maisha haya tulijua iko siku yataisha, lakini nimegundua ni vigumu sana kumaliza hali hii, ikiwa vipato vya wanafamilia havijaimarika ni vigumu sana hali ya namna hii kuisha. sasa tufanyeje ili kumaliza hali hii kwa kifupi Ukiwa kama baba au mama mwenye nyumba ndiye mwenye uamuzi wa kumaliza au kubadilisha hali hiyo hapo kwako.
Binafsi nimeshuhudia baadhi ya familia zikipata taabu kwa ajili ya kuwahudumia ndugu hawa, inapofikia hatua mgeni wa hapo nyumbani kwako unamkabidhi chumba cha watoto wako na wewe unaishia kujibana na watoto kwenye chumba kimoja ukihofia kumlaza yeye na watoto wako hii ni hali mbaya sana.
kwa jinsi maisha yalivyo sasa watu wengi wamekuwa na tabia ambazo hazitabiriki, kiasi zinatisha kwa wewe mzazi kumlaza mtoto wako na mgeni yeyote atayekuja hapo ndani ukihofia jambo lolote baya analoweza kumfanyia mtoto. Hali kama hizi zimepelekea watu wengi kuviacha vyumba vya watoto wao na kuwaachia wageni ambao wamekuja hapo nyumbani kutumia vyumba ambavyo mahususi viliandaliwa kwa ajili ya watoto na kutumiwa na wageni. Na watoto kuendelea kuchangia vyumba na wazazi wao na wasijue ni lini wataweza kuvipata vyumba vyao.
Kwa kweli hali kama hii inarudisha nyuma maendeleo kwani ni ndoto ya kila mzazi kuishi kisasa zaidi namaanisha, kila mtoto kuwa na chumba chake, lakini kwa wakio wengi bado ni ndoto kwa ajili ya ndugu na jamaa ambao wengi wao bado ni tegemezi kwa familia zao.
basi kama wewe ni mmoja wa wageni unaye ishi katika familia za aina hii hebu chukua hatua ya kutafuta ni namna gani utaweza kujitegemea na kuwapa fursa watoto na wanafamilia angalau baada ya miaka kadhaa ya kusota chumbani kwa baba na mama hatimaye warumie vyumba vyao.
Thursday, September 27, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment