Msaidizi wangu ni mkubwa kuliko mimi ,
Wamama wenzangu nakuja kwenu na hoja hii nakomaje!!!!
Nina mama mtu mzima ambaye ananisaidia shughuli za hapa
nyumbani sasa ni mwaka wa pili, watu wananisifu kuwa nimeweza kuishi naye muda
mrefu kwani nikiwa kama bosi naonekana mdogo kuliko yeye kwani ana umbo kubwa
na mungu kamjalia mashalaa.
Ukweli mpaka nimeona nifunguke humu ni kwamba nakuwa kama
namuogopa ukweli ninamuogopa kwani kunabaadhi ya vitu nashidwa kumwambia
ukizingatia kuwa mimi ndio mama mwenye nyumba. Sasa nimekuwa najiuliza nifanye
nini ili niweze kurudisha umama wangu nyumbani kwangu.
Kabla sijawa na huyu dada nilikuwa na dada mwingine mdogo
kiumri na pia alikuwa mdogo kiumbo tofauti na huyu niliye naye sasa. Ukweli
nikilinganisha hapo awali nilikuwa naendana na dada huyu mdogo vizuri ikiwa
kuelekezana hata akikosea niliweza kumgombeza kwamba mbona hapa hivi na pale
vile. Sasa bwana kivumbi kipo hapa kwa huyu mtu mzima kwanza anajiona anajua na
vilevile akikosea kumwambia wewe nakomaje,
naishia kufanya mwenyewe baadhi ya kazi zile ambazo huwa hazifanyi vizuri kwa
kuhofia kumwambia pale anapokose.
Ukweli ni kwamba anafanya baadhi ya kazi vizuri, na baadhi
anakosea ila kwa upande wake yeye anaona ni sawa, Kumuhitaji namuhitaji kwani
sina mtu mwingine wa kunisaidia na vile unajua siku hizi kuwapata hawa akina
dada ni kazi.
Nasikitika pale ninapoona nimekuwa dhaifu wa kumwambia
anapokosea kwa vile namuogopa kwa vile yeye ni mkubwa na mimi ni mdogo, na pia
naogopa akiondoka kwa sasa sina mtu mwingine na mimi ninafanya kazi za
kuajiriwa. Najua wazi mimi ndio boss na ninamamlaka yote ila nashidwa kumkoromea.
Nayeye naona ameshagundua udhaifu wangu huo ananiangalia tu nafikiri ananichora
tu. Mume wangu ananishangaa na ameshawahi kuniambia mbona unamuogopa mfanyakazi
wako kama amekushinda mwachishe kazi .
Marafiki zangu hawajui kero hii ya huyu dada, ila hawaishi
kumsifia kuwa eeh msichana wako ni mchapa kazi kama nini, na wanataka wapate
wamama watu wazimz kama mimi. Nisaidieni jamani nifanye nini?
No comments:
Post a Comment