Zunguka gari yako ,
Hiki si kichekesho wala utani ni kweli kabisa, wewe mama ambaye unaendesha gari au wewe baba unayeendesha gari, ni vizuri kuizunguka gari yako kabla huajaondosha mahali ilipo. Ni kama kuchukua taadhari ili kuepusha vifo ambavyo labda vingezuilika hasa kwa watoto wadogo.
Haikuwa dhamira yake lakini ilitokea kama bahati mbaya, akamkanyaga mtoto amabaye alikuwa nyuma ya gari bila muhusika kufahamu yaani kama laiti yule dereva angezuka ile gari kuangalia kama kuna mtu au kitu chochote karibu na gari angeweza kuepusha kifo hicho.
wanasema ni kazi ya mungu, lakini kunakitu tunaweza kufanya mimi, wewe na yule, hatujazoea sawa lakini tunaweza kukianzisha sasa, ukiwa umepaki gari yako mahali popote tuwe na mazoea angalau kulizunguka kuangali kama kuna kitu au mtu yeyete karibu na gari. Pia kiusama maranyingi mahali tunapoegesha magari huwa kunakuwa na wazi kwa kulikagua na kulizunguka gari lako unaweza kuona kama gari yako iko salama haijanyofolewa taa au kitu chochote zaidi ya yote ndio hilo la kuangalia usama wa watoto wetu.
Monday, October 8, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment