Subscribe:

Ads 468x60px

Wednesday, October 10, 2012

WAJISIKIAJE KUWAMJAMZITO KWA UMRI WAKO MKUBWA

UJAUZITO KWA UMRI HUO?

Kwa siku izi utasikia watu wakisema, ukiwa na umri wa miaka 35 na zaidi si jambo zuri kufikiria kuwa na mtoto, hasa pale ikiwa ndio mara ya kwanza kwa wewe kupata ujauzito na kwa wale ambao wanaendele pia madaktari wanashauri si vizuri sana kubeba ujauzito katika umri kama huo.

Lakini hebu tuangalie kuna ukweli gani,

Ukweli kwa kitaalamu upo, lakini basi mbona tumeshuhudia ndugu jamaa na marfiki wakifanikiwa kupata watoto kwa umri zaidi ya huo naamanisha watu wameweza kupata watoto katika umri mpaka miaka 45.

Ukweli ni kwamba tupo wengi tunahitaji watoto, ila kwa kusoma vitabu mbalimbali, na ushauri mbalimbali zilizotolewa na madakitari kumewatia uoga wamama, wadada wengi kufikiria kupata watoto katika umri zao hizo kubwa walizo nazo.

Mchangia mada mmoja alisema, siku izi tuanaolewa tukiwa na umri mkubwa tofauti na pale zamani, sasa tunafanyaje, ukweli ni kwamba muda mwingi tulikuwa tunaangaika na jinsi ya kuboresha vipato vyetu, na hata hao waoaji huwa wanakuja kidogo umri umekwenda sasa tufanye nini?

Kuna mwandishai mmoja yeye alisema mwisho wa siku ni wewe mwenyewe, kama kwa umri wako huo unayo afya nzuri, unakula vizuri na unafanya mazoezi vizuri hakuna haja ya kutia hofu, wewe kama unahitaji mtoto endelea na mpango wako huo na wala usihofu.

Mama mwingine yeye alisema siku izi kwa umri wake ukiwa mjamzito, hatakiwa kwenda clinic mapema kwani bainafsi anaona ni jambo la aibu kupishana na mabinti wadogo sawa na watoto wake huko clinic.

Ukweli unabakia pale pale wewe unayemtafuta mtoto ndio unajua umuhimu wa hiyo mimba uliyo nayo kwa umri huo, usiruhusu watu wakuamulie, au wakuhukumu, kwani hawakujui na wala hawajui ni kwanini umepata ujauzito katika umri kama huo. Cha msingi wewe be yourself.

kama kuna mwanamke yeyeto ambaye anaumri wa mika 35 na zaidi na ni mjamzito , napenda kukutia moyo, kujitunza, kuangalia unakula nini na ukiweza fanya mazoezi kidogo kidogo ni muhimu sana na usione aibu. Don't listen to judges, Be Yourself

No comments:

Post a Comment