Subscribe:

Ads 468x60px

Friday, October 12, 2012

JE WAJUA

Ukishaolewa kwenu ni kwenda kusalimia tu na si kulala.

Kuna baadhi ya makabila hapa kwetu Tanzania yanamila ambazo hazimruhusu binti kurudi kwao kulala mara akisha olewa, na yapo baadhi ya makabila ni ruhusa unaweza kwenda kwenu kulala hata kama umeolewa ila uwe umepewa ruhusa na mumeo.

Nimepata babati ya kusoma mstari kati kitabu kitakatifu biblia na kugundua kuwa  si sahihi kwenda kwenu kulala mara unapoolewa kumbe makabila hayo yako sahihi kabisa kwa uhondo zaidi hebu zama ndani ya biblia zaburi 45 mstari wa 10-11.

Ni kitu cha kawaida siku izi kuona mabint wengi wakishaolewa kuwaona wapo majumbani kwa wazazi wao kwa vigezo vya kwenda kusalimia, au kwnda kujifungua na mambo mengine madogomadogo,. Imefikia hatua hata mtu akikorofishana na mumewe kidogo solution mtu anapaki mabegi anakwenda kwao

Hebu wewe dada,mama, au bint kaa chini ujiulize, kama kweli ulikuwa tayari kuolewa . Hukatazwi kwenda kwenu ila si kwenda kulala na mji wako unamwachia nani. Nenda salimia kama kuna shida saidi na kisha urudi kwako.

No comments:

Post a Comment