UMEAMUA KUWA MAMA ?
Leo ningependa kuongelea wazo la kuwa mama na unyonyeshaji wa mtoto,
Mpendwa bloger tumesikia watu wengi wakilalamika kuhusu unyonyeshaji pamoja na ulaji ili kupata maziwa mengi, ni vitu vinavyoleta changamoto sana hasa kwa wamama ambao ndio kwanza wanaanza kuwa wamama,
Watu wengi sasa wameamasika kuhusu unyonyeshaji, ila wengi wenapata tatizo ni namna gani wanaweza kupata maziwa mengi ili yamtosheleze mtoto na asitumie maziwa mengine. Ikiwa wewe ni mama ambaye unajua ni jinsi gani hebu tusaidiane katika hili uwe huru kutoa mawazo yako.
Mimi ni mama binafsi nina mtoto ambaye mpaka sasa nina mnyonyesha maziwa yangu, ninachofanya ni kula vyakula vingi vya majimamji pamoja na kunywa maji maji mengi kisi cha lita 2 kwa siku.
Kwa kufanya hivyo imenisaidia sana maziwa ni mengi na yanamtosha mtoto, jopokuwa ninachangamoto moja ambayo ni jinsi mtoto anavyosumbuliwa na gas, colic, ni tatizo ambalo lina wasumbua watoto wengi ila mara nyingi linakwisha mtoto anapofika miezi 3, ila wapo baadhi ya watoto wanakwenda mpaka miezi 7 mpaka 10, hapo pia unaweza kumsaidia mtoto kwa kumtoa hewa mara anapomaliza kunyonya na pia kumlaza kwa tumbo.
WAZO LA LEO,
Mama hebu mnyonyeshe mtoto wako usione haya kutoa nyonyo , kwani si jambo la aibu, pia ukiona vipi tumia kitambaa au kanga kijifunika kumnyonyesha mtoto, kumbuka ni bahati ya kipekee wewe kuwa mama na kuweza kumnyonyesha mtoto wako.
Wednesday, October 9, 2013
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment