Subscribe:

Ads 468x60px

Monday, March 26, 2012

Dada wa kazi za nyumbani

Wengi wetu tunawasaidizi  wanaotusaidia kazi za nyumbani, mara tunapotoka kwenda kwenye shughuli za nje tofauti na kazi za majumbani mwetu.
Kwanza kabisa napenda kuwapongeza akina dada hawa kwa kazi nzuri wanazozifanya, tunapokuwa hatupo majumbani mwetu,
Ingawa wapo baadhi ya wadada hawa ambao si waamunifu, kwenye kazi zao, wapo walio vidokozi, wapo wavivu na pia wapo waongo, lakini basi tunajua kuwa kila mtu anaoudhaifu wake, mara nyingi wa mama wenye nyumba huwa wanachukua hatua za kuwafundisha maadili na tabia nzuri mara wanapoona hawana tabia au maadili mazuri. Na ukipata msikivu anaweza kubadilika na akawa vile wewe mama mwenye nyumba unavyotaka awe.
Sasa Basi mara nyingine jitihada hizo zinaweza kuwa bure ,kwani changamoto inakuja pale mara baada ya kumfunza binti huyo baada ya mwezi tu anakuambia anaondoka au anaweza hata kusingizia kuwa amefiwa au wakati mwingine akasema kuwa anaota ndoto mbaya hivyo ni bora aende nyumbani akatibiwe.
Leo naomba tuzungumze ni namana gani unaweza kukaa na msichana kwa muda mrefu, labda miaka 3, au 2 na hata mmoja,
Wengi wetu tunapata dada lakini baada ya mwezi au wiki anaweza akaaga na kuondoka. Sasa basi wale waliobaatika kukaa na dada zaidi ya miaka 2 hebu basi tushirikishane mnafanyaaje.
Jamani hebu tulijadili swala hili kwa ajili ya familia na watoto wetu.




Kwa wale wenye uzoefu na akina dada hawa je mshara wa dada analipwa na mama au baba mwenye nyumba, maana kuna nyumba nyingine zinamvutano kuhusu ni nani amlipe dada mshahara.




Je msichana wa kazi anatafutwa na nani baba au mama mwenye nyumba?




Je unampa nafasi ya kumsikiliza dada anapokosea kujieleza  kabla hujamuadhibu, au kumfukuza kazi?,





4 comments:

Anonymous said...

inategemea na dada unayempata amepevuka akili kiasi gani na amekuja kwa malengo gani. Dada kama si mkaaji hata umpe nini hakai
Nadhani mama ndio anatakiwa amtafute na kumlipa mshahara dada. baba should stay away from dada ikiwemo hiyo hoja ya kusema baba amlipe mshahara unawajengea ukaribu... weee hatari sana mwanaume ni mwanaume tu

Anonymous said...

Best hata mimi nipo pamoja na wewe wanaume tangulini watafute wasichana wa kazi , hukawii kuletewa mwenzio ndani?????

Anonymous said...

NI KWELI KABISA HAWA WADADA HATA UMFANYIE NINI KAMA SI MKAAJI HATAKAA,MI NAFIKIRI YEYOTE ANAWEZA KUTAFUTA DADA HAIJALISHI ILA SASA AKISHAFIKA KWENYE MSHAHARA MAMA NDIO AJISHUGULISHE NAYE NA SIO BABA. NATAMANI HAWA WADADA WANGEKUWA WANAIHESHIMU HII KAZI NA KUTOKUWA WANARUKARUKA TU, YAANI IWE NI AJIRA KWAO INAYOWAPATIA KIPATO CHA KUTOSHA SI ELF 40 ZAIDI YAHAPO NAO WATOE HUDUMA KWENDANA NA KIPATO CHAO.

Anonymous said...

Ni kweli hawa madada hata kama utamfanya kama mdogo wako wa kuzaliwa nae, kama si mkaaji hakai tuu hata umlipe mshahara mkubwa. Na kutafuta dada ni kazi ya mama na sio baba. Nafasi ya kusikilizwa wanapata.

Post a Comment