Kama utakumbuka baadhi yetu tulipokuwa wadogo, au tuliosoma shule zinazomilikiwa na serikali, tulikuwa tunaadhibiwa kwa kuchapwa viboko, kwemye mikalio au mikononi,
Kwa hivi sasa baadhi yatu tunatumia njia zile zile walizotumia wazazi wetu, kutuonya au kutufundisha kwa watoto wetu wanapokosea.
Sasa basi kitaalam inaonyesha kuonya kwa kuchapa fimbo si sahihi, ni bora kufikiria njia nyingine kabla hujaamua kutumia njia uliyo adabishwa nayo wewe, Kwa sasa kuna njia nyingene za kutoa adhabu kwa watoto tofauti na ilivyokuwa zamani.
Kuchapa kunamadhara kwa watoto, moja wapo ni kumdhalilisha mtoto, hii inamsababishia mtoto kuwa na asira, ukatili, pia inaweza kumsababishaia maumivu makali, zaidi ya yote kama lengo ni kumuonyesha kuwa amekosea ujumbe unakuwa haujafika,
Sasa basi utumie njia gani kumrekebisha mtoto?
Unaweza kumueleza kwa utaratibu kuwa kosa analolifanya lina madhara gani katika maisha yake, kwa kuongea mtoto ataelewa kuwa kosa analolifanya lina madhara kwake.
Pia kumuondolea zawadi mbalimbali ambazo huwa anapatiwa ikiwa atafanya jambo vizuri, huenda akimaliza kufanya homework huwa anaruhusiwa kwenda kucheza mpira, sasa basi kama atafanya kosa unamuondolea hiyo nafasi ya kwenda cheza mpira.
Kama tatizo litaendelea kuwa kubwa ni bora kuonana na dakitari au mtaalamu wa saikologia ya watoto.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment