Subscribe:

Ads 468x60px

Friday, March 30, 2012

PASAKA HIYOOOO YAJA


Kwa wakristo pasaka ni sikukuu ya kukumbuka kufa na kufufuka kwa mwokozi wao, hivyo basi huwa kunakuwa na pilikapilika nyingi kwa ajili ya sikukuu hiyo, watoto huwa wananunuliwa nguo mpya, zawadi mbalimbali, zaidi ya yote wanafunzi pia hufunga shule kwa ajili ya kusherehekea sikukuu hiyo.
wafanyakazi za maofisini alikadhalika huwa wanapumzika pia.

Je ni lazima kumnunulia mtoto nguo mpya kwa ajili ya sikukuu hiyo, au nguo zinunuliwe wakati wowote wa mwaka?

Maana imekuwa kama ni desturi ya wengi wetu kuwanunulia watoto nguo katika misimu ya sikukuu , sasa basi inaweza tokea kwa bahati mbaya sikukuu imefika na wewe huna pesa ya kununulia watoto nguo za sikukuu Utatuaje huo mzozo? maana patakuwa hapotoshi.

Hebu tusaidiane huu mjadala, maana nishaanza ulizwa vipi nguo za sikukuu ? nisaidieni jamani

No comments:

Post a Comment