Subscribe:

Ads 468x60px

Wednesday, March 28, 2012

Unene kwa watoto wadogo ni Afya nzuri au ni tatizo la kiafya


Mdau unaweza kuchangia mada hii, ili tuwekane sawa,

Ni kawaida sana kwa tulio wengi kusema mtoto mnene ndio mwenye afya nzuri, utakuta mtu anafurahia sana akiwa na mtoto mnene sana,
Hebu kwnanza tuangalie ni kitugani kinachangia mtoto kuwa mnene au mtoto kuwa mwembamba.

kwanza kabisa watoto tunaowazaa ni lazima kwa kiasi kikubwa watafanana na wazazi wake, sasa basi unene wakati mwingine unasababishwa na jinsi zilitoka kwa wazazi wa mtoto, kama wewe ni mzazi mnene pia itapelekea kwa kiasi kikubwa mtoto wako kuwa mnene , kama wewe ni mzazi  mwembamba pia mtoto atakuwa mwembamba kama wewe mzazi.

Hivyo basi tusijipotoshe kwa kusema kuwa mtoto wako akiwa mwembamba ati anakuwa hana afya.
kitu cha msingi cha kuzingatia ni kwmba mtoto wako anakula vizuri, na haugui mara kwa mara na pia analala vizuri kielelezo kikubwa ni uzito wake. Utakuta mtoto wako anauzito nzuri na hana unene wala usihofu na usipende kumlinganisha na watoto wa mtu mwingine. kila mtoto anauzuri wake na kila mtoto ni mzuri cha msingi ni kumtunza na kumpenda mtoto wako.

No comments:

Post a Comment