Subscribe:

Ads 468x60px

Tuesday, April 10, 2012

WA MAMA WA LEO WANASEMA!!!!!

Kwa wamama wa leo, tunao wasaidizi majumbani mwetu, ila tusipokuwa waangalifu na kuwa watu tunaofuatilia mambo yanayoendele majumbani mwetu kwa kweli tutajikuta tumefika pabaya,

Tunawapenda sana watoto wetu je unajua ni wakati gani wa kuanza kumshirikisha mtoto wako awe wa kike au wa kiume kufanya kazi ndogo ndogo kama vile, kutandika kitanda chake mwenyewe, kuandaa meza wakati dada au mama anapika chakula, kufua nguo zake za ndani mwenyewe n.k

Unaweza kuanza kumfundisha mtoto kufanya vitu vidogovidogo kwa kuanzia chumbani kwake, akiwa na umri wa miaka miwili unaweza kumfundisha kuokota matoi yake aliyoyasambaza chumbani kwake, kisha unamfundisha kutandika kitanda, na kwa vile anavyozidi kukuwa na idadi ya matoi yanaongezeka ni vizuri pia kumfundisha kutoa zile toi ambazo hazimfai kwa maana amekuwa mkubwa na awapatie watoto wengine wechezee..

Ili kuwatengenezea mazingira ya kujiamini unaweza pia kuwanunulia mbwa, au paka au kuku au mnyama yoyote ambaye wanampenda ili wajifunze kuwajibika, mfano  ikiwa wanapenda mbwa wajitahidi kuhakikisha kuwa huyo mbwa anakula, hapo tayari unakuwa umewafundisha kuwajibika japo si wao walio andaa chakula ila watakukumbusha kumpatia mbwa chakula.,

Wanavyozidi kukuwa wanaweza pia kujiandalia chai, kama kuna snacks za kubeba kwenda nazo shule wataweza kujiandalia pia , inabidi tuwape nafasi na sio kuwaambia we acha, mwambie dada, au dada atafua, sawa dada anaweza kufanya kazi zote lakini unamfundisha nini mtoto wako?

  

2 comments:

Anonymous said...

Kwa kweli watoto wetu inabidi tuwalee kama sisi tulivyolelewa, kwani hata wtoto wa obama sasha na Malia huwa wanafua nguo zao wenyewe, mama yao anasema ukisoma kwenye blog za huko marekani , watoto wake wanafua nguo zao, na pia wanatandika vitanda vyao haoni kwa nini wasifanye hivyo hata kama wapo ikulu. Tuige mfano huo

Anonymous said...

Ukweli ni kwamba kuna akina mama wengine tunajisau, hivi hujawahi kwenda mahali labda kwa rafiki yako ukasikia mtoto wake anavyomwamrisha dada, kama hivi we dada njoo utoe vyombo nimemaliza kula, huyo ni mtoto kwani huyo mtoto angeelekezwa hivi ukimaliza kula peleka sahani jikoni ingekuwaje? mimi naona turudi majumbani mwetu tuangalie

Post a Comment