Subscribe:

Ads 468x60px

Thursday, May 3, 2012

simu ya mkononi noma!!!


SIMU YA MKONONI KWA MUME NA MKE, JE NI SAWA KUANGALIA SIMU YA MWENZIO?

Nisaidieni jamani, mimi ndio kwanza nimeingia kwenye ndoa  ila siku nilipoamua kuolewa na mume wangu nilijua kuwa hakuna siri tena kati yetu sisi kwani ni mwili mmoja sasa,kwa wakristo tunaambiwa kuwa sisi ni mwili mmoja sasa.
Ila kwa upande wangu naona bado hatujawa mwili mmoja, kwani japo najua simu ni private properity ya mtu lakini si kwa mume namke, hebu fikiria unamuona mumeo busy na simu, anatuma na kupokea simu ukimuuliza ati ni marafiki zangu, jamani inakera. Mimi inanikera kiasi kwamba nimeomba ushauri kwa wazoefu wa ndoa,
Binafsi nimesha mwambia mume wangu kuwa, hakuna siri kati yangu mimi nayeye kwani kama alikuwa na mambo binafsi alishayamaliza kabla hajanioa mimi, hivyo sioni sababu kuwa na siri, hii ikiwa ni pamoja na kutoangalia sms zinazotumwa ndani ya simu yake, sio kama si muamini ila nataka kujua ni nani aliyetuma sms ilo tu. Nina haki ya kujua kila kitu kinachoendele katika maisha yake, kama yeye alivyo na wajibu wa kujua maisha yangu pia .
Nisaidieni.  

No comments:

Post a Comment