TOYS TUNAZO WANUNULIA
WATOTO ZINASAIDIAJE ?
Wazazi tunawapenda sana watoto wetu, kiasi kwamba tunapenda
kuwanunulia kila kitu amabacho Wapenda, kuna wakati mtoto anapenda toys
nyingine ambazo zinapelekea kumfanya mtoto afanye au awe na tabia mbaya. Mfano
ukimnunulia toy ya bunduki hapo moja kwamoja unamfundisha kuwa mpiganaji,mgomvi na na wakati mwingine atakuambia nitakupiga bunduki nitakuua na bunduki unaona sasa hii inaonyesha kabisa si zawadi nzuri kwa mtoto ,kwani hivyo ndivyo anavyowaambia watoto wenzake anapokuwa anacheza nao.
Umeshawahi sikia huko nchi za wenzetu, baadhi ya wanafunzi
wamekutwa na matukio mbalimbali ya kutumia silaha wakiwa mashuleni, na wakati mwingine kuzitumia kuwauwa wanafunzi
wanzao.Kitu kama hicho kinakuwa kimeanzia utotoni, labda watoto kama hao walikuwa wakitumia bunduki za toi na kadhalika.
Kitu cha msingi ni sisi wazazi kuangalia ni toys za aina
gani tuwanunulie watoto wetu, hivi ukimnunulia toy ya bunduki unamfundisha
nini?
Hivi umeshawahi kumnunulia mtoto kitabu badala ya toy, tunaamasishana
kusoma vitabu,lakini hatujafanya jitihada za makusudi kuwafundisha watoto
kupenda vitabu kama zawadi na pia kuvisoma pamoja. Hebu kama hujawahi mnunulia
mtoto kitabu kama zawadi siku moja ukasema leo sikununulii toy nakununulia
kitabu na ufanye hivyo marakwa mara kweli utaleta mabadiliko mazuri, Ili kuwa
na kizazi kinachopenda kusoma vitabu ni vizuri sisi wazazi kubadilisha shopping
list na kuongezea kununua vitabu katika list hiyo, Hebu jiulize kama
unavyokwenda shopping huwa unapitia book shop? , umesha wahi kuingia book shop na watoto wako?
Na si kuvinunua tu na kuvisoma pia kama wewe hupendi kusema msomee mwanao.
Tubadilike kwani watoto wetu hujifunza kutoka kwetu.
No comments:
Post a Comment