NI KWELI WATOTO WAWILI TU?
Siku hizi kila mwanandoa utasiki anahitaji watoto wawili tu
ni jambo zuri lakini unauhakika ni wawili tu, au ndio ile watoto wawili wa
ndani ya ndoa na wengine nje ya ndoa. Mimi ni mmoja wapo wa wale wanaosema ni
watoto wawili tu, lakini baada ya kufikiria na kuona mambo mengi nimegundua ni
vizuri kuwa na watoto zaidi ya wawili.
Kwetu tumezaliwa watano na kimsingi, tumekuwa katika maisha
ya kawaida sana na mungu ametujalia tumekwenda shule na sasa tunafanya kazi,
tuna waangalia wazazi na familia zetu and life goes on . tunasaidiana pale
mmoja wetu akikwama ila ni sisi tu tulizaliwa mama na baba mmoja, hakuna cha
mtoto wa mjomba shangazi au baba mdogo ambaye anatoa msaada pale unapopata
tatizo. Hivi ndivyo ilivyo kw siku hizi , tofauti na zamani enzi za mama zetu
na baba zetu undugu ulikwenda zaidi ya ndugu mliozaliwa baba na mama mmoja.
Yaani binamu zako wanakuwa sawa na kaka au dada uliyezaliwa nao.
Mimi baada ya kupitia mapito na kuona jinsi amabavyo undugu
wa siku izi ulivyo yaani ni undugu wa kuzaliwa baba na mama mmoja ndio
unaotambulika kwa sasa . nilirudi na kuiangalia familia yangu nikajiuliza je
siku amabayo sitakuwepo hapa duniani na watoto wangu wawili wapo wenyewe
itakuwaje?
Nikaangalia sisi tulio watano jinsi tunavyosaidina , kushauriana
na n.k niliwaonea huruma watoto wangu wawili ndipo nikapata wazo la kuongeza
mtoto lakini nikawa nimechele umri hauniruhusu sasa basi wewe ambaye Umri wako
unakuruhusu hebu fikiria hili?
Hivi umeshawahi kumuona mama mwenye mtoto mmoja anavyohangaika yaani mtoto huyo ni kama mboni ya jicho, akiugua yeye ndio anaugua yaani anapata taabu mpaka utamuhurumia, hivyo kama mungu amekupa kizazi na unauwezo wa kumtunza mtoto ongeza mtoto mwingine isije kuwa majuto ni mjukuu. Kuna dada mmoja namnukuu alisema hivi
Husbands comes and go, money comes and go but the children they will be there with you forever


