Subscribe:

Ads 468x60px

Friday, July 6, 2012

MTOTO MMOJA TU


NI KWELI WATOTO WAWILI TU?

Siku hizi kila mwanandoa utasiki anahitaji watoto wawili tu ni jambo zuri lakini unauhakika ni wawili tu, au ndio ile watoto wawili wa ndani ya ndoa na wengine nje ya ndoa. Mimi ni mmoja wapo wa wale wanaosema ni watoto wawili tu, lakini baada ya kufikiria na kuona mambo mengi nimegundua ni vizuri kuwa na watoto zaidi ya wawili.
Kwetu tumezaliwa watano na kimsingi, tumekuwa katika maisha ya kawaida sana na mungu ametujalia tumekwenda shule na sasa tunafanya kazi, tuna waangalia wazazi na familia zetu and life goes on . tunasaidiana pale mmoja wetu akikwama ila ni sisi tu tulizaliwa mama na baba mmoja, hakuna cha mtoto wa mjomba shangazi au baba mdogo ambaye anatoa msaada pale unapopata tatizo. Hivi ndivyo ilivyo kw siku hizi , tofauti na zamani enzi za mama zetu na baba zetu undugu ulikwenda zaidi ya ndugu mliozaliwa baba na mama mmoja. Yaani binamu zako wanakuwa sawa na kaka au dada uliyezaliwa nao.
Mimi baada ya kupitia mapito na kuona jinsi amabavyo undugu wa siku izi ulivyo yaani ni undugu wa kuzaliwa baba na mama mmoja ndio unaotambulika kwa sasa . nilirudi na kuiangalia familia yangu nikajiuliza je siku amabayo sitakuwepo hapa duniani na watoto wangu wawili wapo wenyewe itakuwaje?
Nikaangalia sisi tulio watano jinsi tunavyosaidina , kushauriana na n.k niliwaonea huruma watoto wangu wawili ndipo nikapata wazo la kuongeza mtoto lakini nikawa nimechele umri hauniruhusu sasa basi wewe ambaye Umri wako unakuruhusu hebu fikiria hili?

Hivi umeshawahi kumuona mama mwenye mtoto mmoja anavyohangaika yaani mtoto huyo ni kama mboni ya jicho, akiugua yeye ndio anaugua yaani anapata taabu mpaka utamuhurumia, hivyo kama mungu amekupa kizazi na unauwezo wa kumtunza mtoto ongeza mtoto mwingine isije kuwa majuto ni mjukuu. Kuna dada mmoja namnukuu alisema hivi

Husbands comes and go, money comes and go but the children they will be there with you forever

3 comments:

Mom and Toto said...

its nyc

Anonymous said...

ni hakika kabisa usemalo; mimi sina pingamizi, pia mie nina watoto wawili nipo busy sana kuongeza mwingine nakimbizana na umri maana na age nayo imeenda nimebakisha muda mdogo; na naomba sana Mungu anisaidie, halafu tuwe tunachunga sana usemi wa midomo yetu ; mimi kwa kuwa nilikuwa nimechanganya sex basi nikaona nimefika! lakini sasa naomba sana kwa Mungu nicancel maneno yangu kwani tangu nianza kutafuta nishapata two miscarriage, naamini Mungu amenifungua na kunisamehe; sasa nipo busy sana; watoto ni kupanga na ni neema Mungu alituzawadia.

Anonymous said...

umesema neno la maana sana tatizo siku hizi maisha ni magumu na uzazi ni mgumu sana,kila mmoja wetu anataka watoto wake waishi maisha mazuri na kusoma shule nzuri ndio maana inabidi kuzaa wachache ili kuwapa mahitaji yao kwa kiwango tunachofikiria. Nasema uzazi ni mgumu maana wengi wetu huzaa kwa operation hivyo unakuwa na limitation ya idadi ya watoto

Post a Comment