Subscribe:

Ads 468x60px

Tuesday, August 7, 2012

Mpenzi wa blog hii, nimerudi tena,
Napenda chukua nafasi hii kukuomba radhi mpenzi wa blog hii kwani kutokana na mambo yaliyokuwa nje ya uwezo wangu nilikuwa sionekani bogini ila sasa nimerudi tena kuendelea kupeana ushauri na kuelimishana kama ukipata fursa ya kupitia blog hii.

MAZOEZI NI MUHIMU ?

sasa basi leo nimekuja na jambo moja muhimu kwetu sisi akina mama, kwamba hebu tutenge muda wa kufanya mazoezi kwani nimepitia vitabu mbalimbali na kuona kuwa maisha ya mwanadamu hasa kama unataka kuepukana na magonjwa au uzee ambao ungeweza ukauchelewesha  ni muhimu kufanya mazoezi.

utakubaliana na mimi kuwa maisha na ustaarabu wa maisha sasa umebadilika hasa , kama hapo awali ulikuwa unatumia daladala kwenda ofisini sasa unatumia gari, na ukifika ofisini badala ya kutumia ngazi unatumia lifti jamani haya ndio mabadiliko ambayo wengi wetu tunayapitia kila siku na mengine mengi yapo wewe unayajua.

sasa basi tufanye nini, kwa kusema hayo mimi naona zipo juhudi za makusudi inabidi kuzifanya ili tuweze kuishi miaka mingi, ili tuzitunze familia zetu na wale wanaotupenda. Jambo la muhimu la kufanya ni kufanya mazoezi pia kubadilisha ustaarabu wetu wa maisha kwa kubadisha hata jinsi tunavyooandaa vyakula vyetu  pamoja na kufanya mazoezi.

Changamoto wanazozipata wanawake wengi mimi nikiwa ni mmoja wapo ni kuamka asubui, kwa kweli nimezungumza na akina mama wengi na wamesema kuamka asubui ili kufanaya mazoezi ni vigumu sana kwao, pia ikizingatia kuwa wao pia ndio wanaowaandaa watoto kwenda shule na wale wasiotumia mabasi ya shule  inabidi mama wakati akielekea kazini kumpeleka mtoto shule ndio aendelee na shughuli zake. 

mimi nasema hiyo ni sababu tosha ya kukufanya usifanye mazoezi lakini sasa wataalamu wanasema  ni lazima ufanye mazoezi sasa uchaguzi ni wako . Bado ipo haja ya kufanya mazoezi kwani wewe mama ukisema huwezi kuna mama mwingine kama wewe yeye anaweza kitu cha msingi ni kupanga muda wako vizuri.

No comments:

Post a Comment