Subscribe:

Ads 468x60px

Wednesday, August 8, 2012

MAMA TENGENEZA JUICE NYUMBANI

SNACKS KWA WATOTO WA SHULE,
Mama Tengeneza Juice Nyumbani.

Leo naomba nizungumzie kuhusu snacks na vinjwaji  tunavyowafungia watoto wetu kwenda navyo shule,  Naomba sana  kwenu akina mama hebu mnapoandaa hizo snacks au juice mfikirie  hili . je ni muhimu sana mtoto wako aende na juice kila siku , hebu fikiria kumuwekea maji badala ya juice nasema hili kwa sababu watoto wengi wanapata usumbufu wa kuugua matumbo . mtoto wangu alikuwa na hili tatizo lakini nilipobadilisha chakula chake na kuanza kupaki maji na kuachana na juice na soda kweli amepona kabisa haugui tena tumbo na zaidi ya yote anapenda kunywa maji sana .

Wazazi tusipokuwa waangalifu watoto wetu watapata madhara hapo baadae, tuache uvivu tujishughulishe na watoto wetu zaidi kuchunguza wanachokula kila siku, hii ni pamoja na kuacha kuwapatia junk snacks na mengine mengi yanayofanana na hayo.

Kuna baadhi ya watoto wemekuwa na hili tatizo la kutokunywa maji , mimi naona ni tatizo kwani maji ni dawa, wewe mama hebu chunguza watoto wanakunjwa maji au akisikia kiu anaomba juice badala ya maji, ikiwa anafanya hivyo hebu chukuwa hatua ya kubadilisha hilo tatizo.

Juice nzuri ni ile amabayo wewe mama unaiandaa mwenyewe hapo nyumbani, juice ni nzuri kwa afya za watoto wetu, namaanisha juice ile wewe mama, au dada ameiandaa pale nyumbani, tuache uvivu tutumie matunda tuliyo nayo hapa nchini mwetu na tuandae juice zetu sisi nwenyewe, kuna misimu mingi ya matunda kwa hivi sasa kuna watermelons nyingi sana (matikiti maji) , machungwa yapo, embe ndio hizo zaja na mananasi halikadhalika, ukichunguza utakuta mwaka mzima tunamatunda ya kutosha hivyo ni jukumu lako wewe mama hebu chukuwa hatua tupunguze trip za mahosipitali kwa kubadilisha lishe zetu na watoto wetu.

No comments:

Post a Comment