Subscribe:

Ads 468x60px

Monday, July 15, 2013

WAZO LA LEO - BIASHARA IMANI?

Hivi unajua kuwa si kila mfanyabiashara ni mjasiliamali, kwani tumeshuhudua biashara nyingi zilizoanzishwa zikifungwa tu kwa sababu mwenye hiyo biashara amestaafu kazi au amefukuzwa kazi n.k

Swali linakuja kama hiyo biashara inajiendesha na umeichukulia mkopo kwa nini ifungwe mara unapostaafu au kufukuzwa kazi, hebu tuzichunguze biashara zetu ni kweli zinatuingiza kipato na faida au ni bora tu kujiona kuwa na wewe pia umefungua biashara, au ni bora tu umetoka nyumbani na kwenda dukani kwako kama wengine wanavyofanya.

Tusijidanganye kwa kuchukua mshara na kulijaza duka , wakati mahesabu yanaonyesha kuwa hujaongeza faida na mauzo yako yameshuka. Ni bora ukae chini uangalie ni kwa jinsi gani utaongeza mauzo na faida bila kuisaidia kuibusti kwa mshahara wako.

No comments:

Post a Comment