Dondoo za leo kwa akina mama
1 Changamoto tunayoipata sisi akina mama wakati wa
kuwaamsha watoto asubuhi ili wajiandae kwenda shule ni nyingi, sasa basi
tujaribu kuwaamsha kwa taratibu, labda unaweza kumtekenya ili aamuke, sio
kumnyanyua mtoto huku amelala, na kwenda kuakia bafuni maji yakimmwagikia.
2 Ili kuwa
karibu na mwanao, inabidi kuwa na mahusiano mazuri, kama vile kuongea naye,
hebu leo muulize mwanao kwa upendo kama anakitu chochote anataka kukuambia,
nahakika atakuambia vitu vingi sana. Hiyo itamjengea mtoto kujiamini hata akiwa
na watu wengine.
3 Wazazi
mnapokuwa na tofautiana jaribuni
kumaliza tofauti zenu,bila kuwahusisha watoto mojakwamoja, kwani watoto
wakigombana itakuwa rahisi kuwaonya, na kuwaambia kuwa Waige mfano kutoka kwenu
wazazi kwani huwa hamgombani.kwani nyinyi ndio role model wao.
4 Jamani tujaribu pia kuwarisisha watoto maadali
ya dini zetu, tunapowalaza tunawasomea hadithi na mambo mengine mengine, basi
tusisahau kuwafundisha kusali kabla ya kulala,na kabla ya kula, pia
tuwafundishe kuwaamkia wakubwa wao, pia bila kusahau kusema asante
.
5 Je wajua watoto waliochini ya miezi 3, wanahitaji
kulala zaidi ya mara mbili ya wazazi wao, na zaidi sana hulala wakati wa
mchana.
Je wajua kupumua kwa pua ni kiafya zaidi, hebu
tuwafundishe na tuwaelekeze watoto wetu kupumua kwa pua, kwani faida zake ni
kuwezesha hewa tunayoivuta ndani kuwa na joto sawia , navile vile hewa inayo
ingia inachujwa vizuri, tofauti na kuvuta hewa kwa kutumia mdomo, ukitumia
mdomo kuvuta hewa kunakusababishia magojwa yanayosababishwa na hewa, pia allergies.Je wajua tunatakiwa kuwaandaaje watoto wetu
kabla hatujawapeleka hospitali tuwa pamoja upate huo ushauri.
No comments:
Post a Comment