Najua tuko busy na kujiandaa sisi wenyewe, kama ni kwenda kazini au kwenye shughuli za kila siku , ila tumia dakika moja tu uchungulie hilo konteina la mwanao la chakula, ili ujue angalau kama anachokwenda kula shule kime andaliwa vizuri au la.
Kingine, unajua wakati mwingine mtoto anakwenda shule bila kalamu, peni, au penseli, hebu pia chungulia begi la mwanao uone kama amepaki madafutari yake na pia mkebe wa kalamu na rula ameweka, ili akifika darasani anakuwa makini na masomo sio kuanza kuomba peni au penseli.
Umejaribu kufuatilia kuwa mtoto anakula hicho chakula unachomuwekea kwenda nacho shule, wengi hula vyakula vya marafi zao, au wakati mwingine ukimdadisi atakuambia mimi sipendi chakula changu, napenda chakula cha rafiki yangu, labda ni chipsi au biskuti, ila la muhimu hapo hebu ongea na mtoto ujue anapenda nini.
Pia huwa wanapeana majina wakitaniana kutokana na chakula mtoto anachobeba kila siku, mimi wangu anapenda chips hivyo wanamtania mr chips,
sasa basi ikawa ni changamoto kwangu kumbadilishaia mtoto snacks anazobeba, mwingine wanamwita mr kijoti, kwa ajili ya juice anayobeba kila mara.
kama mtoto wako ni mvivu wa kula jaribu kuongea na mwalimu wake atakueleza tabia yake ya kula akiwa shule, usiamini sana atakavyokuambia dada, kwamba leo amemaliza chakual chake chote, kumbe sivyo, hivyo wazazi tuwe karibu pia na walimu wa watoto wetu.
No comments:
Post a Comment