Subscribe:

Ads 468x60px

Thursday, March 22, 2012

Tv,au Luninga ni nzuri Lakini!!!!!


Hapana shaka kuwa TV,video game, na internet ni vitu vinavyotuelimisha na kutufurahisha, ila vikitumika bila kuwa na usimamizi hasa kwa watoto kuna madhara kiafya.

Hii ndio sababu sisi kama wazazi inabidi kufuatilia na kuweka kikomo cha muda kwa watoto, katika kutumia na kuangalia vitu hivyo vitatu.

Muda unaoruhusiwa kwa mtoto kuangalia TV, Video game na internent unatakiwa usizidi masaa 2 kwa siku kwa watoto walio zaidi ya miaka 2,

Kufuatilia na kuweka muda maalum wa kuangalia TV,video game na internet, kuna manufaa kwani pia kutamuwezesha mtoto kuwa na muda wa kufanya vitu vingine kama kusoma, kucheza na marafiki, vitu ambavyo vinamsaidia kuimarisha akili na mwili wa mtoto.

Hebu basi tuangalie ni namna gani tutaweza kuweka kikomo hiki kwa watoto, tukianza na TV.

Weka michezo mingine tofauti na TV, ambayo watoto wanaweza kuicheza kwenye hicho chumba ambacho kuna TV. Vitu kama vitabu vya kujisomea,magazeti ya watoto,toys,puzzles.

Kama TV ipo chumbani kwa watoto, pia iondolewe.

Tuwe na utaratibu wa kuzima TV wakati wa kula chakula.

Usimruhusu mtoto kufanya homework akiwa anaangalia TV.

Ifanye TV kuwa kama zawadi, yaani baada ya kumaliza kufanya, homework au kitu ambacho mtoto anapaswa kukifanya,ndipo utamruhusu kuangalia TV.

Kama kawaida yote haya yatawezekana kama sisi  wazazi tutaonyesha mfano.

Kingine unachoweza kufanya ni kuamua kwa pamoja kwamba TV itakuwa inaangaliwa siku za jumamosi au juma pili. Na sio siku za kwenda shule.

Pendelea kuangalia TV na watoto wako, kama program mnayoingalia imekwisha unaweza kutoa pendekezo, kama watapendele kucheza mchezo mwingine, nawewe pia ushiriki katika huo mchezo.

Baada ya kusema hayo hebu turudi tuangalie kama tayari kuna madhara ambayo yameshatokea hapa kwetu,

Madhara huwezi kuyaona mara moja kwani hata sisi watu wazima tunaweza kuyapata, kama ukijiangalia utakuta pia wewe unalo tatizo kama hili, ila kwa vile wewe ni mtu mzima unaweza kujitambua haraka na ukabadilisha tabia yako ila pia wakati mwingine inakuwa ngumu kwani unakuwa na kitu  wazungu wanasema addiction.

2 comments:

Anonymous said...

Mimi kwa kweli sipendi kabisa kitu ninaitwa TV sitting room,wengine sisi ni wazazi wa ubusy, na kwa kawaida tv nanatakiwa kuangalia na watoto for monitoring purpose hata kama ni programme za watoto, mtu mzima unatakiwa uwe around, kuna mambo nimejifunza kwamba wazazi huwa comfortable wakiwaona watoto wanaangalia cartoon but kuna cartoon nyingine ni mbaya sana tena zina maroho ya ajabu kabisa, hivyo basini vizuri mzazi ku monitor hata cartoon watoto wako wanazoangalia lasivyo unaweza kushangaa mtoto nanafanya jambo baya kumbe ame copy and paste to the real life.

Anonymous said...

Mimi naona kwamba, wazazi tunapaswa kuwachagulia watoto program wanazozitama, hasa pale wanapokuwa wenyewe nyumbani, unaweza weka password kwa zile program unazotaka wasiangalie.

sasa basi changamoto ni pale ambapo sasa ulimwengu wetu umekuwa wa sayansi na tekinologia , utakuta unaweka control kwenye TV, lakini ukurudi kidogo utamkuta mtoto anacheza game kwenye simu yako, hujakaa sawa utamkuta kwenye computer anacheza karata, sasa jamani kila sehemu ni electronics, usipokuwa makini utakuta mtoto wako hajatoka nje tangu asubuhi, anahama kutoka tv, kwenyesimu na kwenye computer sasa tufanyeje???

Na changa moto nyingine ni hii, ukimzuia sana mtoto utakuta hafiti kwenye jamii inayomzunguka, namaanisha kwamba, marafiki zake ,jirani zake wajua sasa huyo wako ukimkataza kila kitu atajionaje?

Post a Comment