Subscribe:

Ads 468x60px

Tuesday, March 27, 2012

Habari za shughuli ndugu wadau, wa blog hii,

Habari za shughuli ndugu wadau, wa blog hii,

 Leo napenda kuzungumzia jinsi gani unaweza kumuacha mtoto wako nyumbani bila kukulia, na ukarudi nyumbani ukamkuta yuko salama kabisa.


Ni kawaida sana kuwaona akina mama wengi wanapotaka kutoka kwenda mahali,kuwatoroka watoto wao majumbani, hii ni kwa sababu watoto wengi wemezoea kukaa na mama zao , hivyo mara wanapoona mama anatoka huwa wajiona wapweke hivyo huwalilia.

Sasa basi kunanjia rahisi kabisa ya kutatua hili tatizo.
Wataalamu wa watoto wanatushauri kwamba ni vizuri kuwaaga watoto  wetu hata kama akiwa mdogo kiasi gani, unaweza kuwa na mtoto ambaye ameshakutambua kuwa wewe ndiye mama yake, watoto huwatambua wazazi hata kwa arufu tu, hivyo ukiwa na mtoto wako labda wa miezi miwili au mitatu, nafikiri huo ni wakati muafaka wa kumuaga na kumwambia mimi natoka na tutaonaa baadaye, nakuakikishia kwa njia hiyo ikiwa ni mazoea yako kuwa unamuga mara unapotoka mtoto wako atazoea hali hiyo na hata kulilia hata siku moja.
Dondoo hii nimeipata kwa rafiki yangu Liez yeye anaushuhuda wa jambo hili zaidi,

2 comments:

Lizzie said...

Ni kweli kabisa, watoto huwa wanaishi kutokana na mazoea. Akijua kuwa mbona mama yangu akiondoka ananiaga na anarudi anakuwa hana wasiwasi kwani anajua utarudi tu.

Kwa safari ambayo naye inamhusu ataona maandalizi tu kuwa leo na mimi natoka na mama, kwa jinsi hiyo anakuwa hana wasiwasi pia kwani anajua leo ni zamu yangu kutoka.

Hii inajumlisha tabia mbali mbali pia- kama vile kuamkia, kusema ahsante, pole, samahani n.k

Anonymous said...

Hebu nisaidieni jamani Shikamoo kwa kiingereza unasemaje? maana mtoto wangu mimi analiuliza ati How do you say shikamoo in English, si unajua tena mambo ya English medium school every time Speak English.
Hapa sasa Mzazi inabidi uingilie kama kwani mwishowe watoto watakuwa hawasalimii watu kisa kiingereza, si unajua tena sisi waswahili lazima japo kidogo tukienzi kiswahili chetu ili tufit kotekote.

Post a Comment