Ni kawaida sana siku izi kumuona mtoto wa miaka miwili akiwa amewekwa dawa, sidhani kama ni kwa uamuzi wake au ni wamzazi wake.
Tunapenda sana watoto wetu wapendeze, na tunawapenda sana lakini sidhani kama kuweka dawa ndio njia pekee ya kumpendezesha mtoto.
Kuna njia kama kumvalisha vibanio hata kama ananywele fupi, kuna kumtoga masikio ,lakini pia outfit ya mtoto wako ikiwa nzuri mtoto anapendeza, au kumsuka rasta bila kuzikaza, na zisiwe nyingi. Check picha hii;
kuna umri ambao watoto wao wenyewe wanapenda kusuka, na pia wanapenda kuweka dawa, kama wazazi tunapaswa kuwashauri watoto kutoweka dawa nywele wanapokuwa bado wapo shuleni, Hii pia inapunguza ngarama kwako wewe mzazi. Mfano hebu muone huyu binti akiwa na nywele zake ambazo hajaweka dawa, zinatamanisha jamani.
Wakati mwingine watoto wanapokwenda shule za bording inatulazimu kuwakata wototo nywele ambazo wao wenywewe hawapendi kuzikata, Kwa kweli kwa binti ambaye anapenda nywele zake huwa anatamani kulia, Kama mzazi inabidi kumuelimisha binti yako ili akubali, kwani elimu ni bora kuliko nywele. Huyo binti hapo alizikata nywele zake japokuwa alizipenda sana hebu ona
5 comments:
sikatai haya unayosema kuhusiana na kusuka na kuweka nywele watoto ila watoto wengine vichwa ngumu, wanang'ang'ania!
mi kuna wakwangu anapenda sana kusuka yani hadi akaenda kwa bibi yaka akaanzia huko kusuka. na ukitaka kumtisha we mwambie naenda kukunyoa nywele, weeeeeeeee!
Kusuka si vibaya ila kuweka dawa, jamani ukianza kumuwe dawa mtoto wa miaka mitatu akifika umri kama wako hiyi ngozi ya kichwa na makemikali unafikiri yatakuwa yamefikia wapi? hebu rudini nyuma kidogo sisi wazazi tulipokuwa wadogo umri kama wao, tulifanyiwa hivyo tunavyowafanyia watoto wetu,
si vizuri kumuweka mtoto dawa, mi kwa ushauri wangu mtoto awe na low cut au asuke nywele zake za asili kuweka dawa na kumsuka mtoto nywele za kimasai ni kumkomaza mtoto kichwa unaweza kumsababishia mtoto madhara ya kichwa.
These days we have soloons ambozo zimespecialise kwa watoto tu, wanajitahidi kuwasuka bila kuwakaza sana so its not bad ila kuweka dawa sio nzuri kwa watoto jameni
Post a Comment