Hebu mzazi mwenzangu changia hili ili tuwekane sawa, mzazi na mtoto wote wanaaondoka nyumabani asubuhi sana, mama anakwenda kazi na mtoto shuleni, ila ni kiasi gani ampatie mtoto ili asishinde na njaa atakapokuwa shuleni?
Kama mzazi hutafurahi mtoto wako ashinde na njaa au ndio utampatia sh 1,000 , kwa kweli ni vigumu sana kufanya mchanganuo ambao utatosha kwa mtoto wako kupata lishe akiwa shuleni.
Wewe mama unampatia mwanao sh ngapi? Changia hili swala na wengine wanufaike
2 comments:
Mimi ntachangia kwa shule za awali. Nadhani inakuwa ni vizuri zaidi kama kuna fungu ambalo mzazi anatoa shuleni ama kila siku ama kwa mwezi kwa ajili ya chakula cha mchana kulikoni kumpatia mtoto pesa ajinunulie mwenyewe chakula kwani mwisho wa siku wanaishia kula chakula "junk" kwani wanashindwa kupanga diet. Kwa snacks zingine na maji/ juice ni bora atoke nazo nyumbani.
Sisi tulisoma shule za akina kayumba mama alikuwa ananipa 500, baadaye akapandisha akawa ananipa sh 1000 enzi hizo ili ninunue mihogo, au juice, lakini kama unavyosema wengi wetu shuleni kwetu walikuwa wanapewa pesa lakini ilikuwa haitoshi, sasa swali linakuja
kwa mama anayefanya kazi ukiwa ofisini unatumia zaidi ya buku hatuoni kama tunawapunja watoto wetu, mimi nafikiria kiwango unachompimia mwanao kilingane na ukweli wa maisha kama kweli tunawapenda watoto wetu.
kwani zaidi ya hapo ndio wananunuliwa chips na watu wengine kwa wale wenye tamaa.
Tufanyeje sasa, mpango wa serikali kuanzisha kuwapa chakula wanafunzi wakiwa shuleni ndio suluhisho.
Post a Comment