Subscribe:

Ads 468x60px

Wednesday, March 28, 2012

JE HUWA UNAMSIFIA MTOTO ANAPOFANYA JAMBO NZURI/JEMA


Wazazi wenye watoto wanaokwenda shule za awali mtakubaliana na hilo, kwani kila siku si ijumaa, siku nyingine mtoto anakua amechoka, saa nyingine anahasira, nakila unapomuandaa kwenda shule, anakuwa hataki, na saa nyingune anakuambia mimi leo siendi shule, Hapa naongelea watoto wa shule ya chekechea.

usipotumia busara utamlazimisha kwenda shule, matokeo yake atakwenda shule huku analia na wakati mwingine amenyongonyea kitu ambacho si kizuri.
Elimu ni nzuri lakini inategemea umri wa mtoto kwa watoto wa shule za nursery bado wana muda mrefu wa kwenda shule hivyo siku mtoto  amechelewa kuamka mpumzishe nyumbani kwani hata huko shule muda mwingi wanakwenda kucheza, na kwa   mtoto anakuwa bado hajaelewa umuhimu wa shule. kufanya hivyo ni ili kuepusha uwezekano wa mtoto kuichukia shule wakati shule ni kitu kizuri.

Leo nilipokuwa nakwenda kazini, nimemuona mtoto wa umri wa miaka 3, akiwa analia tena basi yupo mwenyewe na begi lake la shule sielewi kama alikuwa anakwenda shule au la, jamani tuwasindikize watoto shule, tuakikishe tumewaacha mikononi mwa mwalimu na si kuwaacha watoto wadogo waende wenyewe shule kama huyo niliyemuona leo akiwa analia.

2 comments:

Anonymous said...

ni kweli kabisa si busara kwa mtoto wa shule ya awali kulazimishwa kwenda shule kama hajisikii kwenda kwani itamsababisha achukie shule mapema,

Anonymous said...

mimi nina mtoto wa ndugu yangu ambaye alikuwa akienda chekechea anapigwa na wenzake, akaanza kuchukia kwenda shule, mama yake katika kumdadisi kwanini anachukia shule wakati alikuwa anang'ang'ania kununuliwa begi ili aende shule? akasema kuna mtoto ananipiga shule, kwa hiyo ni vizuri wazazi kuwadadisi watoto wa chekechea na kujua yanayotokea wanapokuwa shuleni ili wasichukie shule.

Post a Comment