Subscribe:

Ads 468x60px

Thursday, April 12, 2012

JE WATOTO WANAOFUATANA NI LAZIMA WAGOMBANE?

Hili ni swali kutoka kwa mdau wa blog hii, yeye ana watoto wake wawili wamefuatana, wa kwanza ana miaka 7 na wa pili anamiaka 6. Anawapenda sana watoto wake hii ni kawaida kwa mzazi yeyote yule kuwapenda watoto wake unconditional ila kitu kinachomsumbua hajui ni namna gani ataweza kuwa control ili wasigombane, 

Huyo mtoto mkubwa yeye mara nyingi ndiye anayeanza uchokozi, anaweza kumpiga mwenzie bila sasabu yoyote, anaweza kumfinya au anamvuta nywele ili mradi tu ni vurugu humo ndani.Kunakuwa na kelele vilio basi hujui hata usaidie yupi.
Ili kuweka mazingira salama inabidi kuwachukuwa wote na kuwauliza kwa nini wanagombana na kusuluisha huo ugomvi, lakini baada ya muda mfupi wanaanza tena. Sasa naomba ushauri wenu wenzangu wenye watoto wanaogombana kama wangu.

No comments:

Post a Comment