TUMWAMBIE AU Atajua mwenyewe!
Jamani ni kitu cha kawaida siku izi kusikia mtu anakuambia unakifua wewe, au una moyo kama unao lengo likiwa akuambie jambo linalokuhusu hasa hasa ni mahusiano kati ya mume wako au mke wako na mtu mwingine.
Nimeshuhudia rafiki ndugu, dada ,kaka na shemeji wakiumizwa na mahusiano yao ya mke au mume, kutokana na baada ya kugundua uhusino uliopo either mume na mwanamke mwingine, au mke na mwanamume mwingine. Muhusika akiwa wa mwisho kabisa kugundua uwepo wa mahusiano hayo, kuna waliochukuwa takribani miaka kadhaa kugundua uhusiano kati ya mwenzi wake na mtu mwingine. Kuna waliopata bahati ya kuwa na watoto wadadisi na wanaogundua mahusiano tofauti kwa wazazi wao ambao pia kwa namna mmoja au nyingine waliwasaidia wazazi wao kugundua mahusiano hayo yasio halali.
Kuna wahusika wengine baada ya kugundua kuwa uwepo wao haujagundulika ndipo wanadiriki kumpigia simu mama mahusika na kumwambia hivi unajua mimi ni mke mwenzio, tena ninauhusiano na mume wako sasa ni miaka kumi , tena tumejenga na tuna mtoto wewe hujui? Tena nishakuja hapo kwako, nikalala wakati wewe umesafiri, na tena kwenye msiba wa mkwe wako nilikuwepo ila ulikuwa unifahamu Just imagine.
Lakini ngoja nikupe moyo jibu ni rahisi (so what???)
Kinachomuumiza ni kwamba wewe rafiki yake ulijua, dada, kaka na wengine mnaomfahamu mlikuwa mnajua juu ya mahusiano ya mume wake na mtu mwingine, hakuna aliye thubutu kumwambia Yule dada, Yule mama, hatimaye siku mmoja anagundua halafu unamwambia sikuweza kukwambia kwani ningevunja ndoa yako, jamani hii ni haki kweli? Hii ni story ya mdau wa blog hii hebu changia tumbambie au atajua mwenyewe?
2 comments:
mimi binafsi napenda sana mtu aniambie nijue, kweli nitampenda sana mtu atakayeniambia. mie ndio mwamuzi wa mwisho na si lazima kuwa ukimwambia mtu eti atavunja ndoa. kama hutaki kujulikana tuma basi hata email msg etc ili mhusika ajue.
magonjwa siku hizi jamani
Ni vizuri kumwambia lakini inategemea na mtu mwenyewe wa kumwambia. Kuna mwingine ukimwambia badala ya kufanya uchunguzi kwa kile alichoambiwa anagomba moja kwa moja na mhusika na kusema nimeambiwa akibembelezwa au kudanganywa kidogo anasema yote.
Post a Comment