Subscribe:

Ads 468x60px

Friday, May 25, 2012

SIMU ZA DHARURA


EMERGENCY CALLS,
SIMU ZA DHARURA,

Wazazi  mshawahi kufikiria kama ajali yoyote ikitokea wewe ukiwa haupo kuna namba za kupiga simu kutoa taarifa, Nafikiri kila mtu anajua namba ya simu 911, lakini si kila kitu au kila ajali unapiga hii namba, Majumbani mwetu tumezungwa na ajali nyingi na kila tukio la ajali linawatu au kampuni inalolishughulikia hivyo ni vema kujua namba hizo
.
Muhimu zaidi kwa wale tunao waachia nyumba wasaidizi, ni vizuri kuziweka namba za simu  mahali ambapo ni rahisi kwa msicha wa kazi kuziona na kupiga mara apatapo ajali yoyote. Wasaidizi wetu pia wanasimu ni vizuri ziwe na pesa ya kupigia na sio kupokelea tu, kwani mara nyingine msaidizi wako atahitaji kupiga simu kama kitu chochote kibaya kimetoke.

Ajali ninazozizungumzia hapo ni kama vile short ya umeme inayoweza kusababisha moto, mtoto kuanguka na kuumia kiasi atahitaji gari ya wagonjwa, mtoto kutumbukia kwenye shimo,kuangukiwa na ukuta, mtoto kupata homa kali sana, kuugua ghafla kwa mtu yeyote kiasi cha kuhitaji msaada, kuvamiwa na majambazi na ajali nyingine ,

Namba zinazojulikana nafikiri ni za Polisi, zima moto na Tanesco, Lakini si vibaya ukaong  ezea namba ya gari la wagonjwa au kampuni yoyote ya ulinzi huwezi jua kama nani atapatikana kama ajali itatokea. Baadhi ya emergency Number ni Ambulance 022-112,Fire 022-112, security companies knight support fire & rescue 0754-777100

Wazazi tunawajibu wa kuchukua taadhari hivyo ni vizuri ujue hizo namba na pia watoto wetu tuwafundishe kujua hizo namba pia.

No comments:

Post a Comment