Subscribe:

Ads 468x60px

Wednesday, May 23, 2012

JE UNAJUA KUWA WATOTO WANAGEZANA TABIA ZAO?


UNAJUWA KUWA WATOTO WANAGEZANA TABIA ZAO,

Wazazi tunajua kuwa watoto wajifunza kwa kuangalia, kufundishwa na kuiga tabia za watu wengine hasa watoto wenzao wanaocheza nao. Mara nyingi sana mtoto atakuja kukuambia mama ninunulie begi kama la rafiki yangu, au viatu kama vya rafiki yangu, hata kama viatu au begi lake halija chakaa, ila ni basi tu wanapenda kuigana, kuna wengine wanadiriki hata kupanga ratiba yao ya week end wakiwa shuleni.

Mtoto anakuambia mama twende labda spurs marafiki zangu watakuwa huko jumapili, na mwingine atakuambia nipeleke sine club nilimwambia rafiki yangu nitakuwa huko. Si vibaya kama unaweza kufanya hivyo mtoto anavyokuambia, ila ni vizuri kuwa makini na ratiba yako ya wiki nzima,Mara nyingi usipofanya hivyo mtoto alivyokuambia anakasirika, hivyo basi ni vizuri kumwambia kwa upendo kwamba kwanini hutafanya hivyo yeye atakavyo, ila ni rahisi kukuelewa kama huwa mnautaratibu wa kupanga ratiba yenu kama familia.Mara zote ni vizuri kumshirikisha mtoto ratiba za hapo nyumbani kama vile watoto wote wanajua kuwa jumatatu mpaka ijumaa ni siku za shule , ni vizuri pia kuwaambia jumamosi mtafanya nini, au jumapili mtakwenda kanisani na baadae mtakwenda wapi, na ukimwahidi lazima ufanye kama hutafanya ni vizuri umwambie pia, ili asikuone muongo, kwani watoto wanaamini wazazi wao wasema kweli daima
.
Kumbe ni vizuri basi kuwa na ratiba ambayo familia inaifahamu na iwe imepangwa pamoja kama familia,ili kuepusha kubadilisha ratiba ambayo huwa mnaifuta. Familia nyingi zinakuwa na utaratibu wa kuwa na familia zao siku za week end lakini huwa imo ndani ya ratiba? au mnaamua tu siku hiyo hiyo kwamba leo twendeni beach,

Unajua watoto ni watu wenye serikali yao ndogo kama wenyewe walivyo, hebu sikia hii story, kuna mtoto wa miaka 8 siku hiyo amerudi shule katika mazungumzo ya kawaida na dada yake nyumbani akamjibu vibaya dada yake, na bahati nzuri mama yake alisikia vile mtoto alivyomjibu dada, Kesho yake mama akamuuliza mtoto mbona jana ulimjibu dada vibaya, mtoto akajibu, unafikiri pale nimemjibu vibaya la, laiti ungejua vile marafiki zangu wanavyowajibu dada zao vibaya ndio ungejua. Mama akamuuliza sasa wewe umejifunza wapi hiyo tabia mtoto akajibu kwa marafiki zangu.

Sasa basi akina mama tuchukue nafasi zetu vizuri hasa kwa kuangalia marafiki za watoto wetu, na vile vile lugha wanazozungumza na wasaidizi wetu nyumbani

No comments:

Post a Comment