Subscribe:

Ads 468x60px

Showing posts with label DID YOU KNOW THIS?. Show all posts
Showing posts with label DID YOU KNOW THIS?. Show all posts

Thursday, June 21, 2012

KWELI NI MTOTO ASIYEKUWA


KWELI MWANAUME NI MTOTO ASIYEKUWA,

Nakumbuka tulishawahi kuongelea kuwa mwanaume ni mtoto asiyekuwa na kwamba wewe mke wake ni sawa na mama yake, rafiki yake na pia ni mke wake. Mwanaume akiwa nyumbani tegemeo lake ni kwa mkewe hasa kwa kila kitu, vitu kama chakula, nguo, usafi utunzaji wa document hasa zinazowahusu hapo nyumbani, vyeti vyake, hati ya nyumba, n.k.
Wanachojua maadamu mama yupo hapo nyumbani yeye ndiye muangalizi wa kila kitu, ataitwa kwenye interview  atakuja atakuuliza wapi vyeti vyangu, mnataka mkopo wa nyumba atakuuliza wapi hati ya nyumba, mnataka lipa bili wapi bili za maji n.k hivyo wewe mama unatakiwa kuwa smart kwani wewe ndiye unayetunza document.

Sasa imefikia hatua mungu amewajalia mnakiwanja mnataka kujenga, hapo tena ni sehemu nyingine wanaume wanahitaji msukumo kutoka kwa wake zao, kwani nimeona na ninaona jinsi ambavyo wanawake wanavyo wasukuma waume zao kuanza ujenzi na kufanya shughuli za maendele kwa ujumla.
Si maanishai wanaume wote wapo wale amboa wakiamua fanya jambo hufanya bila kusukumwa au kukumbushwa na wapo wale ambao wewe mama ukinyamaza tu kama ni mkopo mliuchukua utashaa utapoambiwa umekwisha na mjengo hauja anza. Kimsingi kila mtu amuangalie mwenzi wake na kujua ni mtu wa aina gani? Si vibaya wewe mama ukianza halafu yeye akafuatia, ikiwa unafanya kazi na mnachokiwanja na kila ukimwambia mwenzio tuanze kujenga naye anakuwa kama anapotezea wewe sasa chukua hatua, kama unapesa nunu nondo, mchanga, na kokoto ukiweza nunua na matofali, nakumbia kasha mchukue mwenzi na uende naye huko kwenye site yenu, Kesho yake yeye mwenyewe atatafuta fundi na ujenzi utaanza. 
Imeshatokea hivyo, lengo langu leo ni kukuhimiza wewe mama kuchukua hatua ya kuanzisha jambo ambalo mwenzio bado analivutia pumzi.

Tuesday, May 29, 2012

NAIROBI YALIPUKA TENA


Nairobi yalipuka tena , ila kitu cha kumshukuru mungu hakuna mtu aliyekufa, ila cha kusikitisha ni kuona hali ya majengo na mazingira ya yalivyoharibika, who is behind this this time ?

Friday, May 4, 2012

Makuzi ya watoto yanaitaji uangalifu

wazazi kuna vitu vingi tunakua hatufikirii kama vina effect ila kwa kweli ni muhimu kuwa waangalifu maana vingi vinawaaffect watoto wetu kama sio sasa basi katima maisha yao baadae.

Umewahi kufikiri kwa nini tabia ya kunywa pombe huwa inakua kama ya kurithi kwa watoto wa wanaokunywa? hii ni kwa sababu wengine huwa wanaziona pombe nyumbani na kujua wazazi wake wanakunywa na kwa mtoto kila anachokifanya mzazi ni halali kwake. kwa hivo wengi hujaribu katika umri ambao hawezi kujudge kwamba si kitu kizuri.

Angalia mtoto huyu;

Thursday, April 19, 2012

BED ROOMS FOR GIRLS/BOYS

Kuna mdau mmoja wa blog hii ameomba nimsaidie kuuliza kwamba , ni umrigani ndio haswa unafaa kumtenganisha mtoto kutoka chumbani kwako na kumuwekea chumba chake mwenyewe.


Kwa watu wengine huwa mtoto anakuwa na chumba chake anapokuwa na umri wa miaka mitatu na kuendelea, ila kunakuwa na wakati mgumu kwani inabidi wewe mama katika muda tofauti usiku kwenda kumchungulia na kumuangalia kuwa amelalaje.


Ilikuvutia mtoto apende kuwa na chumba chake mwenyewe ni vizuri kukiwekea furniture zinazovutia pamoja na rangi zinazovutia, Mfano watoto wa kiume wanapenda sana rangi za blue, na watoto wa kike wanapenda sana rangi za pink. hebu tazama hapo chini.




Huwezi amini wapo watoto wanaopenda kuwa na vyumba vyao wenyewe, tena wanadai kabisa, kuna umri mtoto akifika anapenda kuwa na mambo yake mwenyewe, hivyo ni wazo zuri na vizuri tuwasaidie kama uwezo huo upo.

Wednesday, April 11, 2012

MPANGILIO WA WATOTO NA TABIA ZAO




Ni kawaida kwa mzazi akiwa na mtoto zaidi ya mmoja, kuwalinganisha hasa tabia zao, tangu pale walipozaliwa., Utakuta huyu alikuwa analia sana , labda huyu alikuwa analala sana huyu ni mpole au huyu ni mtundu n.k
Hata hivyo  watoto hao  wanapozidi kukuwa tabia na maumbile yao huzidi kutofautiana siku hadi siku. Mara nyingi muonekano wao hutofautiana kiasi kwamba ni vigumu kutambua kuwa  ni watoto wa mama na baba mmoja.
Katika miaka mingi watafiti wemegundua kuwa kuna uhusiano mkubwa wa tabia za watoto na mpangilio wa kuzaliwa. Kwa mfano watoto wa kwanza kuzaliwa,mtoto wa pili, na wamwisho.

Mtoto wa kwanza.
Mtoto wa kwanza katika familia mara nyingi anawajibika juu ya wenzake,anakuwa na mpangilio wa mambo yake,huwa anafanikiwa katika mambo yake, na huwa anonyesha mfano mzuri wa kuwa kiongozi mbele ya wadogo zake. Yeye huwa anakuwa ndiye kinara wa tabia njema au anayefanya vitu ambavyo wazazi huwa wanapenda, na mara nyingi anafanya hivyo kama mfano kwa wadogo zake.kama kuna watoto wadogo hapo nyumbani mtoto wa kwanza anakuwa kama yeye ndio mlezi na wadogo zake wanapenda kujifunza kutoka kwake
Mara nyingi wanakuwa na malengo ya kufanya vizuri shuleni na marazote wanapata mafanikio kwa sababu wanajitahidi sana.Kwa bahati mbaya mara nyingine kwa sababu ya kutaka sana kufanikiwa kunamsababishia msongo wa mawazo ambao si vizuri sana kwa watoto.

Mtoto wa kati
Mtoto wa katikati mara nyingi anachukuliwa kuwa mtoto mgumu sana kumuelewa, Mara nyingi mtoto huyu hapati nafasi ya kupendwa kama alivyokuwa mtoto wa kwanza au wa mwisho, huwa anaona anatengwa na ni vigumu sana kwake kuona ni mwelekeo upi aende. Na mara nyingi anakuwa na mtazamo tofauti wa nini afanye au nani awe, ili kujitofautisha na mkubwa wake,  na mara nyingi huwa ni mtafiti na huwa anapenda kujaribu vitu    ambavyo ni vigumu kujua matokeo yake.

Mtoto wa mwisho
Mtoto wa mwisho ni mtoto wa familia, ni mtoto ambaye kila mmoja ndani ya familia anawajibika kumuangalia. Wazazi wanapenda kumpendelea na mara nyingi zile sheria wazazi walizoweka huwa kwa mtoto huyu wa mwisho azizingatiwi tena.


Tuesday, April 3, 2012

Do you what to win your Wives Husbands... ?

10 things your wife want to hear!

1. “Thanks for all you do for our family.”
Yes, you work hard. You might even feel that your load is a million times heavier than your wife’s. But your wife works hard, too…and a little thanks goes a long way.
2. “You are a great mom and wife.”
If you really want to make her day, go beyond saying “thank you” and praise her for doing a good job.
3. “Let me do that for you.”
Your wife realizes you are exhausted when you get home from work. She probably is too. So offer to help out. Start with something small like cleaning up after dinner. Or, if you really want to score points, do something else you normally don’t do.
4. “I love you so much.”
Did you notice the extra words, after the “I love you?” Telling your wife you love her is a great start, but telling her why you love her, how much you love her, or that you’ll love her forever, will melt her heart.
5. “You are beautiful.”
No matter her age, her size or how long you’ve been married, a woman loves to hear that you think she’s attractive. And, don’t just say, “You look nice.” Instead, use adjectives like, great, lovely, fantastic.
6. “Let me watch the kids.”
If you already watch your children regularly, good job! If you don’t, think of it this way. When you offer to take care of the children, your wife gets to recharge her batteries. A wife with a recharged battery is usually more patient, kind and loving.
7. “Let’s go out tonight.”
Take charge of your next date night. This shows your wife that you enjoy spending time with her.
8. “I’m sorry you had a hard/frustrating/disappointing day.”
These words let your wife know that you are aware of what’s going on in her life.
9. “I would marry you all over again.”
In one sentence you’re telling your wife you value your life together and that you’re committed to her.
10. “How can I be a better husband to you?”
http://www.markmerrill.com

Women are very easy animal to deal with if you know what button to press!  this is almost all that we need guys! ....do your rehearsals on these!

Saturday, March 31, 2012

Je ni sawa kumuweka mtoto dawa kwenye nywele

Ni kawaida sana siku izi kumuona mtoto wa miaka miwili akiwa amewekwa dawa,  sidhani kama ni kwa uamuzi wake au ni wamzazi wake.
Tunapenda sana watoto wetu wapendeze, na tunawapenda sana lakini sidhani kama kuweka dawa ndio njia pekee ya kumpendezesha mtoto.
Kuna njia kama kumvalisha vibanio hata kama ananywele fupi, kuna kumtoga masikio ,lakini pia outfit ya mtoto wako ikiwa nzuri mtoto anapendeza, au kumsuka rasta bila kuzikaza, na zisiwe nyingi. Check picha hii;

kuna umri ambao watoto wao wenyewe wanapenda kusuka, na pia wanapenda kuweka dawa, kama wazazi tunapaswa kuwashauri watoto kutoweka dawa nywele wanapokuwa bado wapo shuleni, Hii pia inapunguza ngarama kwako wewe mzazi. Mfano hebu muone huyu binti akiwa na nywele zake ambazo hajaweka dawa, zinatamanisha jamani.

Wakati mwingine watoto wanapokwenda shule za bording inatulazimu kuwakata wototo nywele ambazo wao wenywewe hawapendi kuzikata, Kwa kweli kwa binti ambaye anapenda nywele zake huwa anatamani kulia, Kama mzazi inabidi kumuelimisha binti yako ili akubali, kwani elimu ni bora kuliko nywele. Huyo binti hapo alizikata nywele zake japokuwa alizipenda sana hebu ona


Friday, March 30, 2012

JE HUWA UNAMSIFIA MTOTO ANAPOFANYA JAMBO NZURI/JEMA



Kila mzazi anatakiwa kumsifia mtoto apofanya jambo, au kitu kizuri, hii itamfanya awe anafanya hivyo mara kwa mara, kwani yeye pia anafurahia pale kila anapofanya hivyo, anapata labda zawadi, au pia special attention from both parents and people around him/her
I
naeleweka kabisa kwamba kila mtu anapenda kusifiwa, hata mimi napenda kusifiwa, recognition, pale ninapofanya zaidi ya kawaida, hivi ni vitu muhimu sana katika maisha ya kila siku.

Vile vile upendo wa wazizi kwa watoto wake haufananishwi na kitu chochote, Mzazi si mpaka akwambie kuwa anakupenda hila katika hali ya kawaida huwezi kufikiria kuwa mama au baba anaweza kumchukia mtoto aliyemzaa mwenyewe. Ila kitalam inabidi utamke kuwa unajua mwanangu mimi nakupenda, kwa kutamka pia inasaidia sana kuisikia ile sauti ikijirudia akilini mwake anapokuwa mwenyewe.

Hebu leo ukirudi nyumbani mtamkie mwanao , unajua nakupenda sana.

MTOTO WAKO ANAONGEAJE BAADHI YA MANENO, TUPOSTIE ILI TUCHEKE PAMOJA.( MISAMIATI YA WATOTO) 

ONLY MOM UNDERSTANDS KIDS

Jamani tunatoka mbali, baadhi yetu, tulipokuwa wadogo mama zetu wanatuambia vile tulivyokuwa tunatamka maneno na wewe unabisha , sasa tumekuwa mama watoto wetu wanataka maneno  visivyo,

Hebu sikia vile Baraka wa Ruth anasema,
Mama  ninue bakeli ingine hii YANUNA ( mama anatafsiri eti baskeli yake ya zamani imechafuka )




Siku ya kuzaliwa (Birthday) kwa watoto huwa ni furaha sana, Baraka akiona keki yeye huimba hivi, papi tu yu,( maana yake Happy birthday to you) inachekesha na kufurahisha, hebu tutumie hivyo vijineno.




Ushawahi ulizwa mtoto ametoka wapi, unajibuje?
Ushawihi kuulizwa kwa nini huendi kwenu wakati kwa baba yako ni pale tu,
kwa wale wanaotumia majina ya waume zao like Mrs Kipara kama kipara is your husband,  hujawahi kuuilizwa kwani wewe kipara ni baba yako au wale watakao kuita mama kipara utaulizwa kwani wewe baba ni mtoto wako .?









Wednesday, March 28, 2012

JE HUWA UNAMSIFIA MTOTO ANAPOFANYA JAMBO NZURI/JEMA


Wazazi wenye watoto wanaokwenda shule za awali mtakubaliana na hilo, kwani kila siku si ijumaa, siku nyingine mtoto anakua amechoka, saa nyingine anahasira, nakila unapomuandaa kwenda shule, anakuwa hataki, na saa nyingune anakuambia mimi leo siendi shule, Hapa naongelea watoto wa shule ya chekechea.

usipotumia busara utamlazimisha kwenda shule, matokeo yake atakwenda shule huku analia na wakati mwingine amenyongonyea kitu ambacho si kizuri.
Elimu ni nzuri lakini inategemea umri wa mtoto kwa watoto wa shule za nursery bado wana muda mrefu wa kwenda shule hivyo siku mtoto  amechelewa kuamka mpumzishe nyumbani kwani hata huko shule muda mwingi wanakwenda kucheza, na kwa   mtoto anakuwa bado hajaelewa umuhimu wa shule. kufanya hivyo ni ili kuepusha uwezekano wa mtoto kuichukia shule wakati shule ni kitu kizuri.

Leo nilipokuwa nakwenda kazini, nimemuona mtoto wa umri wa miaka 3, akiwa analia tena basi yupo mwenyewe na begi lake la shule sielewi kama alikuwa anakwenda shule au la, jamani tuwasindikize watoto shule, tuakikishe tumewaacha mikononi mwa mwalimu na si kuwaacha watoto wadogo waende wenyewe shule kama huyo niliyemuona leo akiwa analia.

Sunday, March 11, 2012

Did you ever wonder how a child ended up with a specific mother


Did you ever wonder how a child ended up with a specific mother? 
According to Sufi mysticism, the soul of the child looks down at the world and 
sees every soul that resides in every woman. When he finds the one that will be 
able to help him fulfill his life's purpose, he makes his choice. The relationship between
 the mother and child is no accident.At times the child may reject his mother and wish he
 had a different one.  Remember your soul made the choice for a reason. 
This woman can help you live your purpose.