Subscribe:

Ads 468x60px

Showing posts with label WOMEN'S CONNER. Show all posts
Showing posts with label WOMEN'S CONNER. Show all posts

Monday, July 15, 2013

WAZO LA LEO - BIASHARA IMANI?

Hivi unajua kuwa si kila mfanyabiashara ni mjasiliamali, kwani tumeshuhudua biashara nyingi zilizoanzishwa zikifungwa tu kwa sababu mwenye hiyo biashara amestaafu kazi au amefukuzwa kazi n.k

Swali linakuja kama hiyo biashara inajiendesha na umeichukulia mkopo kwa nini ifungwe mara unapostaafu au kufukuzwa kazi, hebu tuzichunguze biashara zetu ni kweli zinatuingiza kipato na faida au ni bora tu kujiona kuwa na wewe pia umefungua biashara, au ni bora tu umetoka nyumbani na kwenda dukani kwako kama wengine wanavyofanya.

Tusijidanganye kwa kuchukua mshara na kulijaza duka , wakati mahesabu yanaonyesha kuwa hujaongeza faida na mauzo yako yameshuka. Ni bora ukae chini uangalie ni kwa jinsi gani utaongeza mauzo na faida bila kuisaidia kuibusti kwa mshahara wako.

Sunday, July 14, 2013

NIMERUDI TENA

Haya tena wanandugu nimerudi tena, baada ya kutokuwa na wewe mpenzi wa blog hii kwa muda usiopungua kama miezi 9, Kwa kweli niliwakosa na ninahamu nanyi  ili tujulishane yale yanayotuzunguka katika maisha yetu ya kila siku.
 
Nianze kwa kuwaomba radhi wle niliowakwanza kutokuwa kwangu hewani labda hakuwa wanapata kitu cha kusoma kutoka humu mara waingiapo ndani ya blog hii kweli inaboa nakuomba radhi, lakini nakuomba sasa uendelee kuingia kwani nimerudi kikamilifu sasa.
 yapo mengi ya kujuzana lakini kwa leo ngoja niishie hapo.

Friday, October 12, 2012

JE WAJUA

Ukishaolewa kwenu ni kwenda kusalimia tu na si kulala.

Kuna baadhi ya makabila hapa kwetu Tanzania yanamila ambazo hazimruhusu binti kurudi kwao kulala mara akisha olewa, na yapo baadhi ya makabila ni ruhusa unaweza kwenda kwenu kulala hata kama umeolewa ila uwe umepewa ruhusa na mumeo.

Nimepata babati ya kusoma mstari kati kitabu kitakatifu biblia na kugundua kuwa  si sahihi kwenda kwenu kulala mara unapoolewa kumbe makabila hayo yako sahihi kabisa kwa uhondo zaidi hebu zama ndani ya biblia zaburi 45 mstari wa 10-11.

Ni kitu cha kawaida siku izi kuona mabint wengi wakishaolewa kuwaona wapo majumbani kwa wazazi wao kwa vigezo vya kwenda kusalimia, au kwnda kujifungua na mambo mengine madogomadogo,. Imefikia hatua hata mtu akikorofishana na mumewe kidogo solution mtu anapaki mabegi anakwenda kwao

Hebu wewe dada,mama, au bint kaa chini ujiulize, kama kweli ulikuwa tayari kuolewa . Hukatazwi kwenda kwenu ila si kwenda kulala na mji wako unamwachia nani. Nenda salimia kama kuna shida saidi na kisha urudi kwako.

Wednesday, October 10, 2012

WAJISIKIAJE KUWAMJAMZITO KWA UMRI WAKO MKUBWA

UJAUZITO KWA UMRI HUO?

Kwa siku izi utasikia watu wakisema, ukiwa na umri wa miaka 35 na zaidi si jambo zuri kufikiria kuwa na mtoto, hasa pale ikiwa ndio mara ya kwanza kwa wewe kupata ujauzito na kwa wale ambao wanaendele pia madaktari wanashauri si vizuri sana kubeba ujauzito katika umri kama huo.

Lakini hebu tuangalie kuna ukweli gani,

Ukweli kwa kitaalamu upo, lakini basi mbona tumeshuhudia ndugu jamaa na marfiki wakifanikiwa kupata watoto kwa umri zaidi ya huo naamanisha watu wameweza kupata watoto katika umri mpaka miaka 45.

Ukweli ni kwamba tupo wengi tunahitaji watoto, ila kwa kusoma vitabu mbalimbali, na ushauri mbalimbali zilizotolewa na madakitari kumewatia uoga wamama, wadada wengi kufikiria kupata watoto katika umri zao hizo kubwa walizo nazo.

Mchangia mada mmoja alisema, siku izi tuanaolewa tukiwa na umri mkubwa tofauti na pale zamani, sasa tunafanyaje, ukweli ni kwamba muda mwingi tulikuwa tunaangaika na jinsi ya kuboresha vipato vyetu, na hata hao waoaji huwa wanakuja kidogo umri umekwenda sasa tufanye nini?

Kuna mwandishai mmoja yeye alisema mwisho wa siku ni wewe mwenyewe, kama kwa umri wako huo unayo afya nzuri, unakula vizuri na unafanya mazoezi vizuri hakuna haja ya kutia hofu, wewe kama unahitaji mtoto endelea na mpango wako huo na wala usihofu.

Mama mwingine yeye alisema siku izi kwa umri wake ukiwa mjamzito, hatakiwa kwenda clinic mapema kwani bainafsi anaona ni jambo la aibu kupishana na mabinti wadogo sawa na watoto wake huko clinic.

Ukweli unabakia pale pale wewe unayemtafuta mtoto ndio unajua umuhimu wa hiyo mimba uliyo nayo kwa umri huo, usiruhusu watu wakuamulie, au wakuhukumu, kwani hawakujui na wala hawajui ni kwanini umepata ujauzito katika umri kama huo. Cha msingi wewe be yourself.

kama kuna mwanamke yeyeto ambaye anaumri wa mika 35 na zaidi na ni mjamzito , napenda kukutia moyo, kujitunza, kuangalia unakula nini na ukiweza fanya mazoezi kidogo kidogo ni muhimu sana na usione aibu. Don't listen to judges, Be Yourself

Monday, October 8, 2012

KABLA HUJAONDOSHA GARI HEBU IKAGUE

Zunguka gari yako ,

Hiki si kichekesho wala utani ni kweli kabisa, wewe mama ambaye unaendesha gari au wewe baba unayeendesha gari, ni vizuri kuizunguka gari yako kabla huajaondosha mahali ilipo.  Ni kama kuchukua taadhari ili kuepusha vifo ambavyo labda vingezuilika hasa kwa watoto wadogo.

Haikuwa dhamira yake lakini ilitokea kama bahati mbaya, akamkanyaga mtoto amabaye alikuwa nyuma ya gari bila muhusika kufahamu yaani kama laiti yule dereva angezuka ile gari kuangalia kama kuna mtu au kitu chochote karibu na gari angeweza kuepusha kifo hicho.

wanasema ni kazi ya mungu, lakini kunakitu tunaweza kufanya mimi, wewe na yule, hatujazoea sawa lakini tunaweza kukianzisha sasa, ukiwa umepaki gari yako mahali popote tuwe na mazoea angalau kulizunguka kuangali kama kuna kitu au mtu yeyete karibu na gari.  Pia kiusama maranyingi mahali tunapoegesha magari huwa kunakuwa na wazi kwa kulikagua na kulizunguka gari lako unaweza kuona kama gari yako iko salama haijanyofolewa taa au kitu chochote zaidi ya yote ndio hilo la kuangalia usama wa watoto wetu.


Sunday, September 30, 2012

MSAIDIZI WANGU MTU MZIMA


Msaidizi wangu ni mkubwa kuliko mimi ,


Wamama wenzangu nakuja kwenu na hoja hii nakomaje!!!!
Nina mama mtu mzima ambaye ananisaidia shughuli za hapa nyumbani sasa ni mwaka wa pili, watu wananisifu kuwa nimeweza kuishi naye muda mrefu kwani nikiwa kama bosi naonekana mdogo kuliko yeye kwani ana umbo kubwa na mungu kamjalia mashalaa.
Ukweli mpaka nimeona nifunguke humu ni kwamba nakuwa kama namuogopa ukweli ninamuogopa kwani kunabaadhi ya vitu nashidwa kumwambia ukizingatia kuwa mimi ndio mama mwenye nyumba. Sasa nimekuwa najiuliza nifanye nini ili niweze kurudisha umama wangu nyumbani kwangu.
Kabla sijawa na huyu dada nilikuwa na dada mwingine mdogo kiumri na pia alikuwa mdogo kiumbo tofauti na huyu niliye naye sasa. Ukweli nikilinganisha hapo awali nilikuwa naendana na dada huyu mdogo vizuri ikiwa kuelekezana hata akikosea niliweza kumgombeza kwamba mbona hapa hivi na pale vile. Sasa bwana kivumbi kipo hapa kwa huyu mtu mzima kwanza anajiona anajua na vilevile  akikosea kumwambia wewe nakomaje, naishia kufanya mwenyewe baadhi ya kazi zile ambazo huwa hazifanyi vizuri kwa kuhofia kumwambia pale anapokose.
Ukweli ni kwamba anafanya baadhi ya kazi vizuri, na baadhi anakosea ila kwa upande wake yeye anaona ni sawa, Kumuhitaji namuhitaji kwani sina mtu mwingine wa kunisaidia na vile unajua siku hizi kuwapata hawa akina dada ni kazi.
Nasikitika pale ninapoona nimekuwa dhaifu wa kumwambia anapokosea kwa vile namuogopa kwa vile yeye ni mkubwa na mimi ni mdogo, na pia naogopa akiondoka kwa sasa sina mtu mwingine na mimi ninafanya kazi za kuajiriwa. Najua wazi mimi ndio boss na ninamamlaka yote ila nashidwa kumkoromea. Nayeye naona ameshagundua udhaifu wangu huo ananiangalia tu nafikiri ananichora tu. Mume wangu ananishangaa na ameshawahi kuniambia mbona unamuogopa mfanyakazi wako kama amekushinda mwachishe kazi .
Marafiki zangu hawajui kero hii ya huyu dada, ila hawaishi kumsifia kuwa eeh msichana wako ni mchapa kazi kama nini, na wanataka wapate wamama watu wazimz kama mimi. Nisaidieni jamani nifanye nini?

Thursday, September 27, 2012

Extended Families/ Familia pana

Familia pana au Kubwa,

Familia kubwa hii inamaanisha kuwa na familia zaidi ya mama ,baba na watoto.
Familia nyingi za kiafrika zinaishi na zaidi ya baba,mama na watoto wanasema kwa lugha ya kigeni extended families, Mimi ni mmoja ya watu tulioishi maisha ya namna hiyo nilipokuwa mdogo na mpaka nimeolewa bado naishi hivyo. kwa kifupi maisha ya namna hiyo ni kwa sabababu za umaskini au kipato kidogo kwa baadhi ya familia zetu .

 wengi wetu tuliopitia maisha haya tulijua iko siku yataisha, lakini nimegundua ni vigumu sana kumaliza hali hii, ikiwa vipato vya wanafamilia havijaimarika ni vigumu sana hali ya namna hii kuisha. sasa tufanyeje ili kumaliza hali hii kwa kifupi Ukiwa kama baba au mama mwenye nyumba ndiye mwenye uamuzi wa kumaliza au kubadilisha hali hiyo hapo kwako.

Binafsi nimeshuhudia baadhi ya familia zikipata taabu kwa ajili ya kuwahudumia ndugu hawa, inapofikia hatua mgeni wa hapo nyumbani kwako unamkabidhi chumba cha watoto wako na wewe unaishia kujibana na watoto kwenye chumba kimoja ukihofia kumlaza yeye na watoto wako hii ni hali mbaya sana.

kwa jinsi maisha yalivyo sasa watu wengi wamekuwa na tabia ambazo hazitabiriki, kiasi zinatisha kwa wewe mzazi kumlaza mtoto wako na mgeni yeyote atayekuja hapo ndani ukihofia jambo lolote baya analoweza kumfanyia mtoto. Hali kama hizi  zimepelekea watu wengi kuviacha vyumba vya watoto wao na kuwaachia wageni ambao wamekuja hapo nyumbani kutumia vyumba ambavyo mahususi viliandaliwa kwa ajili ya watoto na kutumiwa na wageni. Na watoto kuendelea kuchangia vyumba na wazazi wao na wasijue ni lini wataweza kuvipata vyumba vyao.

Kwa kweli hali kama hii inarudisha nyuma maendeleo kwani ni ndoto ya kila mzazi kuishi kisasa zaidi namaanisha, kila mtoto kuwa na chumba chake,  lakini kwa wakio wengi bado ni ndoto kwa ajili ya ndugu na jamaa ambao wengi wao bado ni tegemezi kwa familia zao.

basi kama wewe ni mmoja wa wageni unaye ishi katika familia za aina hii hebu chukua hatua ya kutafuta ni namna gani utaweza kujitegemea na kuwapa fursa watoto na wanafamilia angalau baada ya miaka kadhaa ya kusota chumbani kwa baba na mama hatimaye warumie vyumba vyao.

Saturday, August 25, 2012

MASOI SUMAYAN KITCHEN PARTY

Haya tena palikuwa hapatoshi kwa mama Victoria Sumayan  pale nyumbani kwake alipoamua kumuandalia wifi yake Masoi Sumayan sherehe ya kitchen party yaani , kwa kweli shughuli ilipendeza hasa pale unapowashirikisha wanawake wenzako, walikuwepo kama kawaida akina mama wa VG na majirani wengine wengi, mambo yalikuwa mambo, hebu twende tujionee kwa kiasi yaliyo jiri pale nyumbani kwa mama Sumayan.

MASOI SUMAYAN KITCHEN PARTY

 Masoi Sumayan siku ya kitchen part yake ilipendeza sana

 Wakina mama wa VG wakipongezana
Wakina mama wa VG wakiyarudi mangoma

Dada Eve akifungua chamapgne

 Ma MC wa shughuli hiyo wakibadilishana mawazo
 Ehh jirani sherehe imefana

















KWA MAMA SUMAYAN PALIKUWA HAPATOSHI

Ilikuwa ni siku ya furaha kwa majirani na akina mama wa VG kuungana pamoja na kufurahia siku ya kitchen party ya Masoi Sumaiyan kwa kweli tulifurahi sana . Victoria au mama Sumaiyan alitokezea na vazi lake rasmi la huko kwao na alipendeza sana.

Wednesday, August 8, 2012

VG MAMA'S

VG  MAMA'S  SAFARI HII ILIKUWA KWA ROSE













Jumamosi tulikuwa nyumbani kwa Rose ,Maandalizi kwa dada huyu yalikuwa babu kubwa, kama ujuavyo mtu shughuli ikiwa kwako kukaa chini inakuwa nadra , mara umeitwa huku na kule ila mdada alijitaidi kubalance kwa kweli  tulikula tulikunjwa na tulifurahi , na mwisho bila kukosa tulishauriana na kuelimishana kama kawaida kwa akina mama  wanapokutana.

MAMA TENGENEZA JUICE NYUMBANI

SNACKS KWA WATOTO WA SHULE,
Mama Tengeneza Juice Nyumbani.

Leo naomba nizungumzie kuhusu snacks na vinjwaji  tunavyowafungia watoto wetu kwenda navyo shule,  Naomba sana  kwenu akina mama hebu mnapoandaa hizo snacks au juice mfikirie  hili . je ni muhimu sana mtoto wako aende na juice kila siku , hebu fikiria kumuwekea maji badala ya juice nasema hili kwa sababu watoto wengi wanapata usumbufu wa kuugua matumbo . mtoto wangu alikuwa na hili tatizo lakini nilipobadilisha chakula chake na kuanza kupaki maji na kuachana na juice na soda kweli amepona kabisa haugui tena tumbo na zaidi ya yote anapenda kunywa maji sana .

Wazazi tusipokuwa waangalifu watoto wetu watapata madhara hapo baadae, tuache uvivu tujishughulishe na watoto wetu zaidi kuchunguza wanachokula kila siku, hii ni pamoja na kuacha kuwapatia junk snacks na mengine mengi yanayofanana na hayo.

Kuna baadhi ya watoto wemekuwa na hili tatizo la kutokunywa maji , mimi naona ni tatizo kwani maji ni dawa, wewe mama hebu chunguza watoto wanakunjwa maji au akisikia kiu anaomba juice badala ya maji, ikiwa anafanya hivyo hebu chukuwa hatua ya kubadilisha hilo tatizo.

Juice nzuri ni ile amabayo wewe mama unaiandaa mwenyewe hapo nyumbani, juice ni nzuri kwa afya za watoto wetu, namaanisha juice ile wewe mama, au dada ameiandaa pale nyumbani, tuache uvivu tutumie matunda tuliyo nayo hapa nchini mwetu na tuandae juice zetu sisi nwenyewe, kuna misimu mingi ya matunda kwa hivi sasa kuna watermelons nyingi sana (matikiti maji) , machungwa yapo, embe ndio hizo zaja na mananasi halikadhalika, ukichunguza utakuta mwaka mzima tunamatunda ya kutosha hivyo ni jukumu lako wewe mama hebu chukuwa hatua tupunguze trip za mahosipitali kwa kubadilisha lishe zetu na watoto wetu.

Friday, July 6, 2012

MTOTO MMOJA TU


NI KWELI WATOTO WAWILI TU?

Siku hizi kila mwanandoa utasiki anahitaji watoto wawili tu ni jambo zuri lakini unauhakika ni wawili tu, au ndio ile watoto wawili wa ndani ya ndoa na wengine nje ya ndoa. Mimi ni mmoja wapo wa wale wanaosema ni watoto wawili tu, lakini baada ya kufikiria na kuona mambo mengi nimegundua ni vizuri kuwa na watoto zaidi ya wawili.
Kwetu tumezaliwa watano na kimsingi, tumekuwa katika maisha ya kawaida sana na mungu ametujalia tumekwenda shule na sasa tunafanya kazi, tuna waangalia wazazi na familia zetu and life goes on . tunasaidiana pale mmoja wetu akikwama ila ni sisi tu tulizaliwa mama na baba mmoja, hakuna cha mtoto wa mjomba shangazi au baba mdogo ambaye anatoa msaada pale unapopata tatizo. Hivi ndivyo ilivyo kw siku hizi , tofauti na zamani enzi za mama zetu na baba zetu undugu ulikwenda zaidi ya ndugu mliozaliwa baba na mama mmoja. Yaani binamu zako wanakuwa sawa na kaka au dada uliyezaliwa nao.
Mimi baada ya kupitia mapito na kuona jinsi amabavyo undugu wa siku izi ulivyo yaani ni undugu wa kuzaliwa baba na mama mmoja ndio unaotambulika kwa sasa . nilirudi na kuiangalia familia yangu nikajiuliza je siku amabayo sitakuwepo hapa duniani na watoto wangu wawili wapo wenyewe itakuwaje?
Nikaangalia sisi tulio watano jinsi tunavyosaidina , kushauriana na n.k niliwaonea huruma watoto wangu wawili ndipo nikapata wazo la kuongeza mtoto lakini nikawa nimechele umri hauniruhusu sasa basi wewe ambaye Umri wako unakuruhusu hebu fikiria hili?

Hivi umeshawahi kumuona mama mwenye mtoto mmoja anavyohangaika yaani mtoto huyo ni kama mboni ya jicho, akiugua yeye ndio anaugua yaani anapata taabu mpaka utamuhurumia, hivyo kama mungu amekupa kizazi na unauwezo wa kumtunza mtoto ongeza mtoto mwingine isije kuwa majuto ni mjukuu. Kuna dada mmoja namnukuu alisema hivi

Husbands comes and go, money comes and go but the children they will be there with you forever

Monday, July 2, 2012

UMRI WA KUMTAIRI MTOTO

Ni Umri gani muhimu wa kumtairi mtoto wa kiume?

wazazi walio wengi huwa wanapata tabu kujua ni umri gani mzuri wa kumtairi mtoto, binafsi nilijaliwa kumtairi mtoto wangu akiwa na umri wa miezi miwili, japokuwa niliona nimewahi kumbe nilikuwa nimechelewa  , Wapo walio watairi watoto wao wakiwa na siku 7 yaani kama Yesu.

Ukiwa bado hujamtairi mtoto wako mama bado hujachelewa, kunafaida za kumtairi mtoto wako mapema. Kwanza kabisa unamuondolea maumivu makali kwani akitairiwa akiwa mkubwa huwa wanaumia sana. Faida nyingine ni ya kiafya zaidi umewahi sikia watoto wadogo wakisumbuliw na infections kwenye mkojo mara nyingi, utapunguza sana ugonjwa huu ikiwa utamtairi mtoto wako mapema. Zipo faida nyingi hivyo tutaendele tena kukuletea  topic hii.

Thursday, June 21, 2012

OFA BOMBA KUTOKA REX INVESTMENT


WAMAMA JE MWAJUA NJIA MBADALA ZA KUPATA UMEME,
Kuna kipindi hapa Tanzania tulipitia wakati mgumu wa kutokuwa na umeme, kutokana na mgawo ambao  ulisababishwa na kupungua kwa kiwango cha maji na mambo mengine mengi, Ndipo sa watu wakaanza kutafuta njia mbadala za kupata umeme ikiwa ni pamoja na Solar power, inventor ( Backup) na njingine nyingi. Ambazo zilipatikana kwa gharama kubwa.

Leo nimeona niongelee hili swala kwani nimegundua kuwa kuna watu wengi tuliumizwa na swala hili kwa kutugharimu kiasi kikubwa cha pesa kuliko ilivyo staili na ni kwa sababu ya kutokujua kinachoendelea huko madukani na wapi unaweza kupata kwa bei inayofaa na sio ya kuumiza sana.
Jana nilizungumza na rafiki yangu ambaye yeye anafanya kazi kwenye kampuni inayoshughulika na mambo haya ya umeme wa solar ameniambia mambo mengi na zaidi ya yote kilichonivutia zaidi ni Gharama zao.

Kwa kusema kweli nilishtushwa na gharama alizozisema kwani zilikuwa chini kiasi ambacho sikutegemea, kwani nilikuwa najua kuwa kuweka inventor ( Backup) inagharimu si chini ya 4m kumbe si kweli, zaidi ya yote akaniaambia pia Solar power wanayotoa ni cheap na genuine kwani zipo nyingine ni feki. Na unapogharamia ni mara moja tu halafu wewe unaendelea kutumia tu.
Hivyo basi akina mama wenzangu ili kuepukana na kero za kukatikiwa na umeme au kutokuwa na uhakika wa umeme mnaonaje mkafikiria kuweka solar. Kwani mara nyingi umeme ukikatika utakimbilia kuwasha mshumaa, sasa basi ili kuwasha tata za nje na ndani kwa solar unatakiwa uwe na kiasi si zaidi ya 1m. Kwa kiasi hicho utawasha taa za nje zote na ndani na ukiwa na wataalam wao wanauwezo wa kukuunganishai moja kwamoja  inakuwa kama standby generator yaani umeme ukikatika tu solar unaanza kazi yake.
Kwa kweli nawahamasisha wenzungu tujitahidi tuweke solar twende na wakati tupunguze ngarama na ajali zinazoweza sababishwa na mishumaa, hivyo kama utapenda anza kudunduliza sasa, ikifika 1m tu solar inapatikana kwako. Kama ujuaavyo nyumba ni mama umeme wa uhakika Tumia Solar.
Huduma hii inapatikana Rex Investment, wataalamu wa solar Power wenye uzoefu.Wahi kabla mgao haujaanza
Wanapatika hapa hapa Dar es saalam.

Monday, June 18, 2012

CHARITY BEGINS AT HOME


Charity begins at home,

Mwezi huu ulikuwa na sherehe nyingi  moja wapo ilikuwa ni siku ya mazingira duniani, hapa Tanzania pia tullisherehekea sana, ila mimi napenda kuisherehekea kwa kukumbushana jinsi gani tunaweza kuifanya miji yetu kuwa safi, ila napenda usafi wa miji yetu uanzie majumbani mwetu.

Nimekwisha sikia kuna baadhi ya mikoa hapa Tanzania inaongoza kwa kuwa na mazingira safi moja ya mikoa hiyo ni Kilimanjaro hasa mji wa moshi, na mwingine ni Mwanza, jamani Tanzania yetu hii ni kubwa sna ila miji miwili tu ndio imeonekana kuwa safi kweli hebu tubadilikeni.

Kwa kuanzia majumbani mwetu kwa kuwafundisha watoto wetu usafi, wakiwa nyumbani hata pia wakiwa wapo nje ya majumba yao, hii ikiwa ni pamoja na unapokuwa barabarani, au sheleni, Kumfundisha mtoto kutotupa takataka mpaka akutane na mahali penye dust bin, mimi ninahakika tukifanya hivyo tutakuwa na kizazi kisafi hapo baadae na pia nchi safi. 

Saturday, June 9, 2012

FATHER'S DAY


FATHER’S DAY HERE I COME

Mothers let us celebrate this Father’s day.
When is the last time to visit yor father, the world father’s day is 17TH of June, pls do something, If you have some differences this is the time to make piece

What do people do?

On Father's Day, many people make a special effort to visit their father. They often take or send cards and gifts. Common Father's Day gifts are ties, socks, underwear, sweaters, slippers and other items of clothing. Other people give tools for household maintenance or garden work, luxury food items or drinks.

Many Father's Day gifts have slogans such as "The World's Best Dad", "For My Father" or just a simple "Dad" on them.  Photographs of children can be printed on desk calendars, mugs, T-shirts, mouse mats, bags and even ties. Many fathers are expected to take these to the office to remind them of their families while they are working

Some families celebrate Father's Day by planning an outing or weekend trip, perhaps just for the male members of the family. This may be a simple walk in the countryside or a whole planned "experience".  Other families organize a special meal at home or in a pub or restaurant. A common Father's Day meal is a traditional roast dinner with meat, stuffing, potatoes and vegetables, which can be eaten in a pub and accompanied by pints of ale or lager.

Sunday, June 3, 2012

KITOVU CHA MTOTO, NA URIJALI?


KUNA UHUSIANO GANI KATI YA URIJALI NA KITOVU CHA MTOTO,

Nimesikia wazazi mbalimbali wakiongele swala la kitovu cha mtoto mchanga kudondokea kwenye uume wa mtoto kuwa unaleta madhara hapo baadae, Eti wanasema mtoto huyo ambaye kitovu chake kilidondokea kwenye uume wake atakuwa si rijali je kuna ukweli hapo?
Pia nimeona wazazi walimuwekea kidoti cheusi mtoto mchanga kwenye paji ati, kuzuia kwikwi inahusu vipi? Kumvalisha mtoto kitambaa chausi mkononi au kiunoni jamani inakuwaje, zaidi ya yote mtoto akiwa na kikoozi ambacho hakijapona kwa muda kidogo wanasema anakimeo?
Inakuwaje wewe mama umetoka kujifungua na unapelekwa kwa wazazi wako ati ukale uzazi kwa muda wa miezi 3, na huyo baba uliye zaa naye unamwacha ati hana uzoefu, kwani wewe unao, huoni kama unawasumbua wazazi wako, wakulee wewe na kisha wakulelee mwanao na zaidi ya yote ukae huko miezi zaidi ya 3 , sasa huyo baba mtoto atajua lini kulea mtoto mchanga, Baadhi ya watoto wachanga huwa wanalia sana usiku hivyo vilio huyo baba takuwa amevisikia saa ngapi kwake inakuwa ni adithi tu, mtoto ni wenu wote lakini kusota usiku kubembeleza mtoto usote mwenyewe na wazazi wako hebu fikiria. Kuna baadhi ya akina baba hawataki hata kuwashika watoto wao ati wanadai wanaona kama wanawaumiza jamani hutaki kushika mtoto wako mwenyewe?
Mimi ninaonelea hivi, mara mtu unapojifungua maadamu umeolewa na mumewako yupo hapo ni vizuri ukae hapohapo na usiende popote, mujifunze wote kwa pamoja kumlea mtoto wenu. Wewe mama unatakiwa ufanye juhudi za makusudi kumshirikisha mumeo sio unaambiwa tu nenda kwa mama ndio anajua na wewe unakubali, Ikiwa mtahitaji msaada wa kulea ni bora msaidizi huyo aje hapo kwako na akuelekeze nakisha aende. Zaidi ya yote madakitari wa watoto wapo kila kona hivyo usihofu kuwa jasiri.

Friday, June 1, 2012

ANAJUA KUSEMA ASANTE, KUSALIMIA JE?


MWANAO ANAJUA KUAMKIA NA KUSEMA ASANTE,

 Katika mila na desturi zetu watanzania tunatakiwa kuwafundisha watoto wetu tabia ambazo zinakubaliwa na jamii zinazotuzunguka. Moja ya tabia hizo ni tabia ya kusalimia, na kusema asante.
Kwa kweli usipomfundisha mtoto wako angali mdogo tabia hizi itakuwa ni vigume kuzifanya anapokuwa na umri mkubwa au hata kama atakuwa anasalimia ni mpaka akumbushwe. Hivi umeshawahi kutana na rafiki au jamaa na mtoto anakakataa kusalimia , unajisikiaje kweli inatia aibu mwenzenu yalinikuta .
Kwa kweli inapendeza sana mtoto anapokuwa na tabia nzuri, inapendeza pale unapompatia zawadi, au unapomfanyia kitu mtoto akasema asante, au nyie mwaonaje , Mimi imenisumbua sana kwa mtoto wangu alikuwa hawezi kumsalimia mtu bila kumwambia , mara nikutanapo na rafiki ,jamaa au ndugu kweli ilikuwa inani aibisha kwani ni mpaka aambiwe hujambo,  ndio naye atajibu sijambo, halafu inabidi umwambie tena sema shikamoo, ndi atasema shikamoo, kweli inatia aibu.
Sasa basi siku mmoja akaniuliza hivi mama how do you say shikamoo in English?
Kwa wenzetu wa ulaya wanapenda sana kusema sorry au, neon please, au kindly, au excuse me, haya ni maneno mazuri ya kuonyesha unyenyekevu na kujali mtu mwingine, mara nyingi mtumiaji wa maneno haya, anatumia pale ambapo anataka kufanya jambo au afanyiwe jambo, lakini anajua wazi kitu atakachokifanya kinaweza kisiwe kizuri kwa mtu mwingine, au kikamkwaza mtu mwingine, hivyo kwa kujali hali hiyo  na ndio maana atatumia maneno haya.
Kwetu sisi pia kuna baadhi ya  watu wanayatumia maneno haya pia pale tu anapozungumza kiingereza ila anapozungumza Kiswahili mara nyingine watu wanajisahau kutumia maneno kama haya ambayo ni, samahani, tafadhali, 

Wednesday, May 30, 2012

UKIWA NA KIPATO KIKUBWA NI TATIZO?


MAMA AKIWA NA KIPATO KIKUBWA KULIKO BABA KATIKA FAMILIA NI TATIZO,

Katika pitapita zangu, nime gundua kuwa mama akiwa na kipato kikubwa kuliko baba katika familia ni tatizo kubwa kwa kwa baadhi ya familia.
Binafsi nime shuhudua mama akijishusha sana ili kuchukua nafasi yake ya kuwa mtiifu kwa mume wake hata kama kipato chake ni kikubwa kuliko cha mume wake. Lakini basi bado inakuwa ni tatizo kwani mume Yule mwenye kipato kidogo bado anajisikia kutawaliwa, kutoheshimiwa na kudharauliwa. Mwingine anakuwa mkali na kudiriki kusema au kwa vile wewe unapata pesa nyingi, naona hunieshimu hata kidogo, Wanaume hawa wanakuwa walalamishi sana hata ukifanya kitu kidogo  cha maendeleo nyumbani basi atalalamika hujanishirikisha,
Kuna baadhi ya wanaume huchukua nafasi hii ya kutoelewana na kuanzisha mahusiano mengine ya familia na mwanamke mwingine ambaye yeye anajiona kuwa juu zaidi kipesa, sasa basi anaishia kuwa na familia mbili yaani ya kwa mke wake wa ndoa ambaye kwake yeye anamfanya benki anakuwa anachukuwa pesa na kwenda kuilea ile familia ndogo aliyonayo. Hebu tuchangie hili .


Tuesday, May 29, 2012

LOOk what is Happening in Zanzibar

ZANZIBAR KUNA NINI?


Huwezi amini ili ni swali  anajiuliza kila mtu, anayependa amani, jamani mbona hatujazoea vitu hivi, akina mama na watoto je wanakimbiaje, hebu ona . Iko njia nzuri tu ya kutatua au kurekebisha pale ambapo hapakosawa hebu tuzungumzeni.