Kwa watu wengine huwa mtoto anakuwa na chumba chake anapokuwa na umri wa miaka mitatu na kuendelea, ila kunakuwa na wakati mgumu kwani inabidi wewe mama katika muda tofauti usiku kwenda kumchungulia na kumuangalia kuwa amelalaje.
Ilikuvutia mtoto apende kuwa na chumba chake mwenyewe ni vizuri kukiwekea furniture zinazovutia pamoja na rangi zinazovutia, Mfano watoto wa kiume wanapenda sana rangi za blue, na watoto wa kike wanapenda sana rangi za pink. hebu tazama hapo chini.
Huwezi amini wapo watoto wanaopenda kuwa na vyumba vyao wenyewe, tena wanadai kabisa, kuna umri mtoto akifika anapenda kuwa na mambo yake mwenyewe, hivyo ni wazo zuri na vizuri tuwasaidie kama uwezo huo upo.
1 comment:
Asiyekuwa na uwezo wa kukaa hata vyumba viwili afanye nini? Maana maoni haya ni kwa wenye uwezo tu!
Post a Comment